26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Siri ya Mbowe kuongoza Chadema miaka 15

Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM

ZIMEBAKI takribani wiki mbili kabla ya Desemba 18 ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kitafanya mkutano wake mkuu ambao pamoja na mambo mengine utafanyika uchaguzi wa  viongozi wa juu wa chama hicho.

Mpaka sasa Freeman Mbowe ambaye amekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 15, bado anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huu wa mara ya nne tangu mwaka 2004 alivyoingia kwenye uongozi mara ya kwanza baada ya kupigiwa kura za ndiyo na hapana.

Mbowe ambaye ni miongoni mwa waasisi vijana wa Chadema tangu mwaka 1992, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa mara ya kwanza mwaka 2004 akichukua nafasi ya marehemu Bob Makani.

Kabla ya hapo Mbowe mwaka 1992 alipewa jukumu la kuongoza kurugenzi ya vijana wa chama hicho kwa miaka kadhaa, lakini pia alikuwa mtu muhimu katika utekelezaji wa masuala ya michakato ya ujenzi wa chama na ushauri wa usimamizi wa fedha.

ALIVYOWAIBUA KINA ZITTO

Freeman Mbowe (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe (kulia)

Kutokana aina ya siasa zake, Mbowe ameweza kuibua vijana mbalimbali na kuwakuza kwenye siasa, ingawa baadhi yao walijikuta kwenye mtafaruku naye na baadaye kuhama chama.

Mmoja wa vijana hao ni Zitto Kabwe, ambaye licha ya kukulia Chadema na kuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri, sasa ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.

Mwaka 2004 alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chadema, Mbowe alifanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na mifumo ya uendeshaji wa chama hicho, nembo ya Chadema na zaidi alitaka vijana wapewe nafasi katika chama ngazi za wilaya, mikoa na taifa hasa makao makuu. 

Katika hilo, alifanya ziara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuangalia vijana machachari, wazungumzaji na makini.

Mbowe aliona na kuridhishwa na Halima Mdee (Mbunge wa Kawe kwa sasa) , Zitto Kabwe, John Mnyika na baadaye David Silinde na wengineo ambapo aliwaomba na kuwashawishi kujiunga na Chadema. 

Uwezo wake huo mkubwa wa kuibua vipaji, ni moja ya …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles