22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Siri ya mabao ya Dilunga, Mkude hadharani

Theresia Gasper -Dar es salaam

BEKI wa Simba, Shomari Kapombe, amesema mbinu mbadala walizopewa na kocha wao, Sven VanderBroeck ndiyo siri ya ushindi walioupata dhidi ya Mbao FC.

Simba ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Mbao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kapombe alisema wapinzani wao walikuwa bora zaidi  sehemu ya kiungo hatua iliyowalazimu kupitisha mipira pembeni, mbinu iliyowawezesha kupata mabao hayo.

“Tumeweza kupata ushindi kwa kutumia uzembe wa wapinzani wetu na kupata nafasi ya kufunga mabao mawili, licha ya mchezo kuwa mgumu tuliweza kupambana kwa dakika 90,” alisema.

Alisema kwa sasa wanaendelea kupambana kwa mechi nyingine zinazowakabili mbele yao, ili waendeleze ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa wanaoushikilia.

Simba inakamata uongozi wa msimamo wa Ligi Kuu ikijikusanyia pointi 38 katika michezo 15 iliyoshuka dimbani,  ikishinda12 , sare mbili na kupoteza mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles