26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Siri ya Chuo Kikuu Harvard kuendelea kung’ara duniani

o-HARVARD-UNIVERSITY-facebook

NA FARAJA MASINDE,

MEI mwaka huu ilitolewa orodha mpya ya vyuo vikuu bora duniani na Times Higher Education (THE) huku ikizingatia sifa za chuo kikuu husika.

Hata hivyo jambo la kushtua katika orodha hiyo ni kuwa hakuna chuo hata kimoja kutoka Afrika kilichofanikiwa kuwapo kwenye orodha hiyo ya 100 bora kinyume na matarajio ya wengi.

Vyuo vikuu kutoka Bara la Asia vimeonekana kupiga hatua kubwa mwaka huu ambapo imeingiza vyuo vikuu 17 kwenye orodha hiyo ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na vyuo 10 pekee kutoka barani humo.

Kwa mwaka huu kwa mara ya kwanza kuna Chuo Kikuu cha Tsinghua kutoka nchini China ambacho kimeshika nafasi ya 18.

Hata hivyo katika orodha hiyo vyuo vikuu vya Marekani bado vinatawala vikiongozwa na Chuo Kikuu cha Harvard ambacho kimekuwa na umaarufu mkubwa duniani.

Marekani imefanikiwa kuingiza vyuo vikuu 42 kwenye orodha hiyo idadi ambayo imeshinda vyuo vya Ulaya na Asia.

Chuo cha Harvard

Chuo cha Harvard ambacho ni chuo binafsi kilichoanzishwa mwaka 1636, ada yake kwa mwaka wa masomo 2015/16 ilikuwa ni dola 45,278 ambazo ni sawa na Sh milioni 90.

Kuna sababu nyingi ambazo zinakifanya chuo hicho kuendelea kuwa bora duniani. Miongoni mwa sababu hizo ni uwepo wa wakufunzi mahiri na wanaozingatia wakati.

Mkuu wa Kitivo cha Elimu chuoni hapo, Katherine Merseth, anasema wanafunzi wengi wanaojiunga na chuo hicho hupewa motisha kubwa hali inayowafanya kufanya vyema na hivyo kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho duniani kote.

Lakini pia wanafunzi hupewa fursa ya kusikilizwa zaidi ikiwamo pia katika eneo la kufanya tafiti. Hata hivyo chuo hicho kimekuwa na mkakati wa kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanahitimu na kupata kazi.

“Sababu nyingine inayofanya chuo chetu kuwa bora ni Jiji la Boston ambako ndiko kiliko chuo hiki na kila mwaka huongeza fungu kwenye bajeti yake ya huduma za jamii na hivyo kufanya maisha kuwa rahisi hata kwa wanafunzi wanaofika hapa.

“Chuo hiki kimeiletea heshima kubwa Marekani hivyo serikali imekuwa ikiweka mkazo kuhakikisha huduma zinaimarika licha ya kuwa si chuo cha serikali,” anasema Merseth.

Anabainisha kuwa chuo hicho kina maktaba kubwa zaidi duniani ambayo ina kila aina ya vitabu na kwamba baadhi ya vitabu vilivyopo hapo ni nadra kuvipata kwenye vyuo vingine.

“Sababu zingine zinazotufanya kuwa bora ni namna ambavyo wanafunzi wengi wanaokuja hapa wanakuwa huru kuelezea maoni na mitazamo yao juu ya njia bora za mwelekeo wao wa maisha jambo ambalo halipo kwenye vyuo vingine, wengi wanazingatia tu ada ya mwanafunzi bila kuangalia iwapo elimu yake inaweza kumsaidia ama la.

“Viongozi wakubwa akiwamo rais wa taifa hili, Barack Obama na viongozi wengine wastaafu wa ndani na wa mataifa mbalimbali wamesoma hapa jambo linaloongeza heshima ya chuo hiki, hata rais Obama ameamua kumruhusu binti yake, Sasha kuja kusoma hapa na tayari tumempokea hivyo hii inakuwa ni chachu ya kuendelea kuwa bora,” anasema Merseth.

Anaongeza kuwa madarasa ya chuo hicho yamejengwa kisasa zaidi na hivyo kuwa rafiki kwa wanafunzi wengi wanaofika hapo kutoka mataifa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles