SIRI, FAIDA YA KUAJIRI WATU WALIOSOMA KIMATAIFA

0
626

Na Joseph Lino,

KWA kawaida waajiri huwa wanaangalia mtu mwenye uwezo uliojaa ubunifu na ujuzi wa uzoefu katika utendaji mahali pa kazi.

Jambo hili huleta ushindani miongoni mwa wafanyakazi ambapo kila mmoja hujaribu kuonyesha uwezo na ubora wa kazi yake kwa mwajiri.

Kuna siri na fursa kwa upande wa wanafunzi wa kimataifa kutokana na uzoefu pamoja na  ujuzi maalumu ambao huwafanya watambulike kuwa wafanyakazi bora kati ya wengine.

Kwa upande mwingine inaweza kuwa vigumu, hivyo unapoandika wasifu wako (CV) na kukutana na waajiri, ni vizuri kujua mambo ambayo yatawafanya wakuone wewe ni muhimu zaidi kwao.

Hizi ni faida nne na siri ambazo wanafunzi wa kimataifa wanavyo, ambazo unapaswa kuzionyesha wakati wa kuzungumza na waajiri.

Wewe ni tofauti

Kama ni mwanafunzi ambaye umesoma vyuo vya nje wanaamini kuwa utaleta mawazo mapya na mtazamo tofauti katika sehemu yako ya kazi na kufanya mwajiri wako kukuona tofauti zaidi na vizuri. Utafiti umeonyesha kuwa taasisi nyingi ambazo zina baadhi ya wafanyakazi waliosoma taaluma nje nchi huwa na ubunifu na maendeleo.

Unajitoa katika kazi yako

Waajiri wengi huamini kuwa mwanafunzi wa kimataifa akae muda mrefu katika kazi moja, lakini wewe binafsi unakuwa umejitoa katika kufanya kazi kwa bidii kwa sababu umetafuta kazi kwa moyo wote.

Hivyo, unatakiwa  ufanye kazi kwa juhudi na kukabiliana na changamoto mbalimbali ili uendelee kuwapo kazini kwa sababu unashauku na motisha ya kuleta mabadiliko kwa kutumia ujuzi na ubunifu wako.

Una mtaji wa kitamaduni

Kama ilivyo kawaida, mwanafunzi wa kimataifa huwa wanajua lugha zaidi ya moja, pia wana uelewa mpana wa mambo mengi ya nje, hiki kinafanya mwajiri kukupa thamani kwenye kazi yako.

Kwa mfano, katika nchi ya Australia kuna kiwango kidogo cha watu wanajua lugha zaidi ya mbili kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Hii ni fursa zaidi kama unafanya kazi na taasisi ambazo zinajihusisha na biashara ya kimataifa.

Vile vile kuwa na ujuzi maalumu ikiwamo utamaduni, uchumi au uzoefu wa kazi kutoka nchi nyingine. Kama mwanafunzi wa kimataifa, utamsaidia mwajiri wako katika ushindani wa kibiashara  na masoko ya nje au wateja.

Umekomaa

Kitu  muhimu zaidi kwa wanafunzi wa kimataifa ni kukomaa na maisha, kwa sababu tayari kila kitu ulikuwa unafanya mwenyewe, uzoefu wa kuishi mbali na nyumbani hadi kufika chuo kikuu mwenyewe na kujitegemea.

Aidha, mwanafunzi wa kimataifa anakuwa amejifunza ujasiri, maadili ya kazi, pamoja na uwezo wa kufanya kazi na watu ambao ni tofauti.
Hii ina maana kwamba ni nadra kumwangusha mwajiri wako kipindi ambapo vitu haviendi sawa na kazi, kwa sababu mwanafunzi wa kimataifa  anakuwa mfanyakazi wa kujitosheleza katika kufanya kazi mwenyewe na ambaye anaweza kufanya kazi vizuri na wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here