29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Sintofahamu yaendelea kesi ya Rugemalila

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili mfanyabiashara, James Rugemalila na wenzake imeendelea kuzua sintofahamu, upelelezi haujakamilika na washtakiwa hawajui hatima ya mazungumzo ya kumaliza kesi hiyo waliyofanya na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Hayo yamebainika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ulipokuwa inatajwa.

Kutokana na sintofahamu hiyo Mahakama imeutaka upande wa mashtaka kufuata sheria, taratibu  na kuzingatia haki za binadamu wanaposhugulikia kesi za washtakiwa mbalimbali mahakamani.

Hakimu Shaidi amesema hayo wakati akitoa uamuzi wa hoja za mawakili wa utetezi waliolalamikia  kucheleweshwa kwa upelelezi na Mazungumzo ya kufanya makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

“Mawakili wote wamekuwa  wakilalamikia kucheleweshwa kwa kesi, imefikia wapi  na kupelekea mshtakiwa Herbinder Seth na Joseph Mwakandege kuandika barua ya kutaka kufanya mazungumzo na DPP.

“Washtakiwa  wamefata utaratibu wa kisheria. DPP hana neno sahihi kwamba kakataa au kakubali na kwa bahati mbaya kanuni za mazungumzo hayo (pre bargain) zilizotungwa hazielekezi cha kufanya baada ya siku 30 za mazungumzo zinazotolewa na mahakama kumalizika.

 “Katika kesi hii nimetoa siku 45, tutaendelea na hili hadi lini?, sote ni binadamu tunapaswa kushugulikiwa kwa heshima na haki za binadamu, nahisi kufanya hivyo kwasababu sio jambo jema,  sisi wote ni watumishi wa umma, leo upo katika nafasi hii lakini kesho hautokuwepo, ni vyema kila mmoja ashugulikiwe kwamujibu wa sheria na taratibu,” amesema Hakimu. 

Hakimu amemtaka Wakili wa Serikali Wankyo Simon kushugulikia suala hilo kwa ukaribu. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 6 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo,Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya  uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha Serikali hasara ya dola za Marekani  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles