24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Singida imepokea chanjo 30,000

Na Mwandishi Wetu, Singida

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge, amewataka wananchi kujikinga na ungojwa wa covid 19, huku akibainisha kuwa Mkoa umepokea chanjo zaidi ya 30,000.

Dk. Mahenge ametoa maelekezo hayo leo, alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja lililopo   Kata ya Msingi, Wilaya ya Mkalama mkoani humo.

Amewataka wananchi hao kujikinga na kuendelea kupata chanjo ambazo serikali imeshazisambaza maeneo mbalimbali mkoani hapo kwa kuwa ni salama kwa afya.

Aidha amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuendelea kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya Corona kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Amewataka madiwani kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu misongamono ambayo sio ya lazima ili kuepuka usambazaji wa ugonjwa huo endapo mtu mmoja atakuwa ameathirika.

Katika hatua nyingine amewaagiza TANROAD kumaliza haraka ujenzi wa daraja unaoendelea katika  Kata ya Msingi ili kurahisisha mawasiliano  katika maeneo mbalimbali  kabla msimu wa mvua haujaanza.

Amesema daraja hilo likikamilika litahudumia mikoa ya Mwanza, Simyu na Manyara.

Aidha amewapongeza viongozi wa TANROAD Mkoani hapo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huo na kuwataka kuhakikisha daraja likamilika kwa ubora na muda uliopangwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles