30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Simu ilivyofanikisha kumkamata aliyemuua bosi wake kwa shoka

Kulwa Mzee -Dar es salaam

WAPELELEZI katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa mfanyakazi wa ndani, Oliana Shabani, anayedaiwa kumuua bosi wake kwa kumpiga na shoka waliyokuwa wakipasulia kuni, wameeleza walivyomkamata mshtakiwa.

Askari hao walitoa ushahidi kwa nyakati tofauti jana katika Mahakama Kuu iliyoketi katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Mpelelezi kutoka kitengo cha upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Koplo Ismail alidai walifanikiwa kumkamata mshtakiwa kwa kuwa alikuwa akitumia simu ya marehemu na ilikuwa hewani.

Shahidi huyo ambaye ni mtaalamu wa makosa ya mtandao, alidai marehemu alikuwa akiitwa Slyvester Njau na Aprili 9 mwaka 2014 akiwa ofisini kwake, mkuu wake wa kazi alimweleza kwamba kuna mtuhumiwa wa kesi ya mauaji yupo Arusha, hivyo wanatakiwa wakamkamate.

Alidai, Aprili 14, akiwa na Sajenti Silviana, walienda Arusha kumfuata mshtakiwa na kwamba ilikuwa rahisi kwao kumkamata kwa sababu aliondoka na simu ya marehemu na ilikuwa hewani akiendelea kuitumia.

“Tukiwa Arusha pia tulipata namba ya James Mbise ambaye alikuwa akiwasiliana na mshtakiwa, alitueleza mshtakiwa ni rafiki yake na amemwacha nyumbani anafua nguo.

“Tulifanikiwa kumkamata mshtakiwa eneo la Kwamromboo na tulipofanya upekuzi tulipata vitu mbalimbali kama mtandio, simu aina ya Nokia, mkoba, vyote mali ya marehemu,” alidai.

Vitu vingine ni kadi ya benki, kamera aina ya Sony, funguo sita za geti na baada ya upekuzi huo walichukua vitu vyote pamoja na mshtakiwa wakarudi naye Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, Oliana anadaiwa kumuua Slyvester eneo la Vingunguti, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles