30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

SIMCU yamsaidia mtoto mlemavu wa miguu Baiskeli

Derick Milton, Simiyu

Chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU) kimetoa baiskeli kwa mtoto mlemavu wa miguu Ritha Elias (8) Mkazi wa kijiji cha Old Maswa Halmashuari ya Mji wa Bariadi.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya msingi ya walemavu ya Matumaini iliyopo jijini Dar es salaam, ambapo baikeli hiyo imegharamu kiasi cha sh. 400,000.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Emmanuel Mwerere alisema kuwa mbali na baiskeli hiyo chama hicho kimetoa Sh 300,000 kwa Ritha ikiwa ni ada ya shule.

Aidha Mwerere amesema kuwa chama hicho kimeamua kumsomesha hadi mwisho mtoto huyo ambaye amezaliwa akina hana miguu na amekuwa akilelewa na bibi yake Pepetua Mtaima.

“ SIMCU katika bajeti yake imetenga kiasi cha sh. Milioni 36.7 ambapo tumepanga kutumia kusaidia sekta ya elimu na afya, akiwemo mtoto huyu kumsomesha mpaka mwisho,” amesema Mwerere.

Akiongea mara baada ya kupokea msaada huo Bibi wa mtoto huyo Pepetua, alishukuru sana SIMCU kwa msaada huo ikiwa pamoja na kujitolea kumsomesha kwani ameangaika sana kuhakikisha mtoto wake anapata elimu.

“ Nimekuwa mtu wa kutangatanga kila sehemu kutafuta msaada ili mjukuu wangu aweze kupata elimu tu, na amekuwa mtoto mwenye akili nyingi darasani mpaka sasa amefika darasa la tatu, nawashukuru SIMCU kwa kujitolea kumsomesha,” amesema Bibi huyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles