27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBACHAWENE: SERIKALI ITAIMARISHA KILIMO

Na FLORENCE SANAWA-LINDI


WAZIRI wa Tamisemi, George Simbachawene, amesema Serikali imejipanga kuwekeza katika sekta ya kilimo ili kiweze kukuza uchumi kama inavyotakiwa.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya Nanenane kitaifa, Kanda ya Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Simbachawene, sekta ya kilimo nchini bado ni mhimili wa uchumi wa nchi kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia 65.5 ya Watanzania na inachangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula hapa nchini.

Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali imeendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, mifugo na uvuvi ili kuweza kuchochea na kufikia uchumi wa viwanda kama Serikali ya Awamu ya Tano inavyosisitiza.

Simbachawene alisema uzalishaji wa mazao ya chakula nchini uliongezeka mwaka 2016 hadi kufikia kiwango cha utoshelevu wa asilimia 123 ingawa mwaka huu utoshelevu huo umeongezeka hadi kufikia asilimia 120.

“Hii sekta ya kilimo si ya kuchezea kwani tumeona sehemu zenye kambi za jeshi wakifanya vizuri katika kilimo kwa kutumia ujuzi wao.

“Kwa hiyo tunaomba watoe elimu kwa wananchi wanaoishi karibu na kambi hizo ili waweze kunufaika na kuanza kuchangia katika sekta hii muhimu nchini.

“Serikali imeweka mikakati mizuri ya kuhakikisha inainua sekta ya kilimo nchini kwa kuongeza mikakati ya kukuza sekta hiyo ili kuchochea uchumi wa kilimo ambao kwa sehemu kubwa unachangia kwa kasi pato la Taifa,” alisema Simbachawene.

Katika hatua nyingine, waziri huyo alizungumzia sekta ya uvuvi na mifugo ambapo alisema Serikali imeendelea kusimamia sheria na kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji nchini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles