27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Simbachawene: Jitokezeni kwenye zoezi la Sensa ili muhesabiwe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amehimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akitoa taarifa muhimu kwa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Simbachaweneameyasema hayleo Agosti 23, 2022 baada ya kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

“Unapohesabiwa unakuwa upo katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa ujumla,” amesema Sinbachawene.

Amefafanua kwamba usipohesabiwa, unakosa fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya mipango ya maendeleo.

“Bado tuna siku tano mbele kwa ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa kuamkia Agusti 23, 2022,” amesema Simbachawene.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene akiwa  katika picha ya pamoja na makarani wa Sensa ya watu na Makazi.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles