Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amehimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.
Simbachaweneameyasema hayleo Agosti 23, 2022 baada ya kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
“Unapohesabiwa unakuwa upo katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa ujumla,” amesema Sinbachawene.
Amefafanua kwamba usipohesabiwa, unakosa fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya mipango ya maendeleo.
“Bado tuna siku tano mbele kwa ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa kuamkia Agusti 23, 2022,” amesema Simbachawene.