31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene awahakikishia mabalozi uchaguzi huru, haki

Na Mwandishi wetu -Dar es Salaam

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amefanya mazungumzo na baadhi ya mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini na kuwahakikishia Tanzania ipo salama na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki.

Mabalozi waliofanya naye mazungumzo ni Kaimu Balozi wa Marekani, Dk. Imni Patterson, Manfredo Fanti (Umoja wa Ulaya – EU), Sandro De-Oliveira (Angola) na Mubarak Alsehaijan (Kuwait).

Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dar es Salaam jana, Simbachawene alisema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini. 

“Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali la hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakuwa wa huru na haki,” alisema Simbachawene. 

Pia aliwahakikishia ushirikiano zaidi kati ya wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

“Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” alisema Simbachawene. 

Aliwashukuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumwona wanakaribishwa ofisini kwake.

“Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote. Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Simbachawene.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles