27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Simbachawene apongeza utekelezaji wa Operasheni Anwani za makazi Kibakwe

Na Mwandishi Wetu, Kibakwe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene akikagua operesheni ya anwani za makazi katika Kijiji cha Mpwanila kata ya Luhundwa katika jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

“Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kujua katika ramani mahali, mitaa, barabara zilipo. Mmefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuja kujifunza hapa,” amesema Simbachawene.

Simbachawene ameyasema hayo Julai 10, 2022 katika ziara aliyoifanya kwenye kata za Pwaga na Luhundwa alipotembelea na kufanya mikutano.

“Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya Postikodi ili Watanzania wajulikane wanakaa wapi; jambo la kuweka mitaa, lakini pia barabara na namba kwenye nyumba katika Halmashauri wilaya ya Mpwapwa na jimbo la Kibakwe limefanyika kwa mazingira makubwa,” amesema Simbachawe.

Waziri Simbachawene ameendelea kufanya ziara kwenye kata mbalimbali zinazounda jimbo hilo la Kibakwe ambayo inaenda sambamba na kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles