23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Simbachawene amlilia Anna Mghwira

Safina Sarwatt, Moshi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa pole kwa msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira.

Salamu hizo amezitoa leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa huo, kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Mkuu wa Mkoa.

Simbachawene amesema alipokea taarifa za kifo cha Dkt. Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa akikumbuka mchango wake mkubwa ambao aliutoa katika ujenzi wa Taifa.

Marehemu Dk. Mghwira aliwahi kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha upinzani AC-Wazalendo  ambapo alikuwa mwanamke pekee kati ya wagombea urais katika uchaguzi huo wa mwaka 2015.

Waziri Simbachawene yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi ya siku siku mbili ambapo atatembelea shule ya Polisi Moshi, Magereza, chuo cha Uhamiaji (TRITA)Jeshi la zima moto, Jeshi la Polisi pamoja na mpaka wa Holili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles