27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene amkubali Kamishna Jenerali Magereza

Mwandishi wetu, Morogoro

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema kasi ya utendaji kazi wa Kamishna Generali wa Jeshi la Magereza Nchini, (CGP) Suleiman Mzee, imemfurahisha kutokana na mabadiliko makubwa ya maendeleo kwa kipindi cha muda mfupi tangu alipoteuliwa kuliongoza jeshi hilo.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua mashine ya kuchimbia ‘excavator’ iliyofanyika Gereza la Mbigili, Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, Simbachawene alisema Jeshi la Magereza lilinufaisha wachache katika kipindi cha nyuma, lakini tangu kuteuliwa kwa CGP Mzee, mafanikio makubwa yameanza kuonekana.

“CGP tangu ateuliwa kwa muda mfupi tuu, amenunua matipa matatu, basi la timu ya mpira na mashine hii excavator kwa fedha zilizopatikana ndani ya jeshi, haya mambo yalikuwa ni ndoto jamani, utendaji kazi wake mzuri na anania ya kuleta mabadiliko zaidi ndani ya jeshi hili la Magereza, nimefurahishwa sana na utendaji kazi wake na fikisheni pongezi zangu,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, askari na maofisa wa jeshi hilo nchini, hawapaswi kumpinga, wanapaswa kumuelewa na kumuunga mkono na kuendana na kasi yake katika kipindi hiki ambacho jeshi hilo limeingia vitani kwa ajili ya kufanyika kwa mabadiliko makubwa.

Pia aliwataka askari Magereza kuendelea kufanya kazi usiku na mchana na kila mtu akitoka kazini ajiulize nini amefanya kwa siku hiyo na kwamba hatua hiyo itawezesha jeshi kubadilika zaidi katika uzalishaji na pia maisha ya askari nayo yatabadilika.

Aidha, Simbachawene katika hafla hiyo, ameitambulisha kauli mbiu mpya ya jeshi hilo ambayo inasema ‘Magereza Tanzania, fikra mpya, mtazamo mpya, kuchapa kazi kwa bidii na kujitegemea.’

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi hilo (SACP), Ismail Mlawa, alimshukuru Simbachawene kwa jitihada zake za kuliletea mabadiliko jeshi hilo na kumuomba Rais John Magufuli amrudishe katika Wizara hiyo baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

“Tunakushukuru sana kwa kuja kuzindua mashine hii mpya, na pia hizi ni jitahada zako pamoja na Afande Kamishna Generali wa Jeshi hili, tunaamini nawe umechangia kupatikana kwa mashine hii pamoja na vifaa vingine, tunakuombea urudishwe kuiongoza Wizara hii hata baada ya uchaguzi,” alisema Mlawa.

Naye Mkuu wa Gereza la Mbigili, lililopo Wilayani Mvomero, Mkoani humo, SSP Muyengi Burilo, alisema mashine iliyozinduliwa ilinunuliwa Sh milioni 331,060,800 na itakuwa inachimba visima, kung’oa miti, kuchimba mitaro na itakodisha katika taasisi mbalimbali za Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles