24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Simbachawene alia na gharama za uzalishaji umeme

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM), amesema gharama za uzalishaji wa umeme kwa sasa ziko juu, hivyo Serikali inatakiwa kuliangalia jambo hilo wakati ikielekea katika uchumi wa kati.

Kauli hiyo ameitoa bungeni leo Jumatano Mei 28, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2019/20.

Aidha, mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, amesema umeme utakuwa na tija kama utaenda katika huduma za kijamii na shughuli za uzalishaji.

“Gharama za uzalishaji ziko juu tunaposema uchumi wa viwanda hatuwezi kufika bila ‘kudeal’ na jambo hili.

“Hizi kelele zipo tu tusibadilishe mwelekeo sababu ya kelele, kuna nchi gani inaupinga huu mradi wa Stigglers Gorge, tunaomba waziri kanyaga mafuta twende mbele,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles