Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amepokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Bunge wa Saba kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ramadhani Suleiman.
Akizungumza wakati wa kupokea Jedwali hilo Septemba 2, 2022 Waziri Simbachawene amesema Serikali inaongozwa na sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo inaweza kutatua changamoto zote zinazogusa watu katika maswala ya sheria; kanuni, taratibu, mila na desturi zinazoongoza Serikali, alisema Waziri Simbachawene,” amesema Simbachawene.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Ramadhani Suleiman amemshukuru Waziri wSimbachawene kwa kupokea Jedwali hilo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba pamoja na majibu aliyoyatoa kwa Kamati ya Bunge.