26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene ahimiza wananchi wa Kibakwe kushiriki Sensa ya Watu na Makazi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene ametoa rai kwa Watanzania kujiandaa kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ikiwa ni pamoja na kuwa na kumbukumbu ya taarifa za watu waliolala katika makazi yao usiku wa kuamkia Agosti 23, 2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene akizungumza na wananchi wa kata ya Mbuga katika jimbo lake la uchaguzi.

Rai hiyo Julai 8, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji cha Mbuga jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Amesema Sensa ya watu na makazi inasaidia serikali kupata idadi ya watu na kupanga mipango ya miradi ya maendeleo kulingana na uhitaji.

“Hata kama watu watatoka ni vizuri anaebaki nyumbani akabaki mtu mwenye kumbukumbuku za watu waliolala katika nyumba yake ili kupata takwimu sahihi.

“Naomba muendele kuwafahamisha wale ambao hawafahamu ili nao wawe na ufahamu na tuendelee kukumbushana kadri tunavyoelekea kwenye zoezi hili la sensa,” amesema Simbachawene.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Sh milioni 100 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu, barabara.

Awali, katika salamu za shukrani Mkuu wa shule ya sekondari Mbuga, Mwalimu Justine Maganga ameshukuru Waziri Simbachawene kwa miradi ya ujenzi wa madarasa matatu na madawati 150 pamoja na viti vyake.

“Nitoe rai kwa watendaji kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ili ujenzi wa miundo mbinu uendane na thamani ya fedha iliyotolewa, kuwe na Mtu maalumu anayesimamia ili aweze kuutolea taarifa sahihi inapohitajika alisema Waziri,” amesema Simbachawene.

Pia ukarabati wa jengo la Maabara ya fizikia na Kemia pamoja vifaa vyake, jambo ambalo limewezesha wanafunzi kufanya mafunzo ya vitendo katika masomo hayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akifurahia ngoma ya utamaduni ya Mangala katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mbuga kata ya Mbuga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akimjulia hali mgonjwa katika Kituo cha afya cha Saint Gema kilichopo Kijiji cha Lumuma.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles