25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yatoa milioni 10 hospitali Mwananyamala

Na Mwandishi Wetu

Uongozi wa Klabu ya Simba umetoa kiasi cha fedha sh milioni 10 katika Hospitali ya Rufaa  Mwananyamala  kusaidia afya ya mama na mtoto.

Simba imetoa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kilele cha Simba Day, Septemba 19,2021  kama  ilivyo kawaida ya kila mwaka hutoa kwa jamii yenye uhitaji.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez amesema mwaka huu wametumia  fedha badala ya vitu ili kutoa wigo kwa uongozi wa hospitali kununua vitu ambavyo vinahitajika kwa haraka.

“Uongozi ndiyo unajua kitu gani kinahitajika kwa haraka na kiasi cha fedha tulichotoa kitasaidia sehemu fulani ingawa tunajua hakitaweza kumaliza kabisa tatizo,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Katibu wa hospitali hiyo, Lilian Mwanga ameupongeza uongozi wa klabu ya Simba kwa  msaada huku akitaka uhusiano huo kuendelea na usiishie hapo na  fedha hizo zotatumika kama ilivyokusudiwa.

“Kwa niaba ya uongozi wa hospitali naipongeza Simba kwa msaada huu, mnaweza kuuona kama ni mdogo lakini kwetu ni mkubwa na tutaenda kuutumia kama ilivyokusudiwa na tunawakaribisha wakati mwingine,” amesema Lilian.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles