30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

SIMBA, YANGA USO KWA USO CECAFA KAGAME CUP

Na LULU RINGO


RATIBA ya CECAFA Kagame Cup imetangazwa rasmi leo na timu ya Simba na Yanga zimepangwa kundi moja. Timu hizo zimepangwa kundi C lenye timu kutoka Ethiopia na Somalia.

Kupangwa huko kundi moja kwa Simba na Yanaga kumepokelewa tofauti na mashabiki wa timu hizo wakidai huenda zimepangwa hivyo kutokana na waandaaji kuhofia timu moja inaweza kutoka mapema bila kucheza na mpinzani wake.

Ratiba hiyo imetolewa na kwa ushirikiano wa TFF, CECAFA na  Azam Media mbele ya waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Regency Hotel ulioko Mikocheni Dar es Salaam.

Mara nyingi tumezoea katika mashindano mengi Simba na Yanga zikipangwa makundi tofauti ili kufanya mashindano mengi kuwa na ladha pale timu hizo zinapoendelea kusalia katika mashindano hali inayofanya timu hizo kukutana katika fainali nyingi kutokana na ubora wa vilabu hivyo.

CECAFA itahusisha timu 12 huku Tanzania mwenyeji akipewa nafasi ya timu 3 moja ikiwa ya upendeleo ambayo imepewa Simba huku Yanga akishiriki kama Bingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita na Azam kama bingwa mtetezi wa kombe hilo mwaka 2015.

“Tumechagua Simba ili kuleta msisimuko zaidi kutokana na kuwa mabingwa wa msimu huu” alisema raisi wa TFF Wallace Karia alipokua akijibu swali la mwandishi mmoja lililokua likisema “Kwanini nafasi hiyo amepewa Simba na si timu nyingine”

Mashindano hayo yanatarajiwa ikuanza rasmi Juni 28 hadi Julai13 ikiwa na makundi matatu huku kila kundi likiwa na timu 4. Makundi hayo na timu zake ni kama ifuatavyo; Kundi A zitazikutanisha Azam FC (Tanzania), Uganda (Reps), JKU (Zanzibar), Kator FC (S.Sudani).

Kundi B linahusisha timu ya Rayon Sports (Rwanda),Gor Mahia (Kenya), Lydia Ludic (Burundi), Ports (Djibut) na Kundi C litawakilishwa na Yanga na Simba (Tanzania),St George (Ethiopia) na Dakadaha (Somalia).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles