24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Simba, Yanga Oktoba mosi

simba na yanga

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limetangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara msimu wa mwaka 2016/2017, huku ikizipanga timu za Simba na Yanga kukutana Oktoba mosi katika mchezo wa mzunguko wa kwanza utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TFF kupitia kwa Ofisa Habari wake, Alfred Lucas, michuano hiyo itaanza rasmi Agosti 20, ambapo mechi saba zitachezwa kwenye viwanja tofauti ukitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Agosti 17.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa ratiba imezingatia michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za Taifa, ili kukwepa dhana yoyote ya upangaji wa matokeo na kurundikana kwa michezo.

“Hii ni ratiba rasmi ukiachana na ile ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, tunaomba familia ya soka kuegemea kwenye hii ya sasa rasmi inayotolewa na TFF.

“Ile ya mitandao ya kijamii imekosewa anuani ya Posta ya TFF, kadhalika kuonesha kuwa mchezo kati ya Azam FC na African Lyon ungefanyika Agosti 21, 2016 ilihali hii rasmi ina anuani sahihi na mchezo huo wa raundi ya kwanza ukionesha utachezwa Agosti 20, 2016,” alisema.

Hata hivyo, katika ratiba hiyo Yanga itacheza na Azam Oktoba 16 ikiwa ugenini, wakati Simba wao watakutana na Azam Septemba 17.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles