Simba, Yanga ngoma ipo pale pale

0
1268

Theresia Gasper -Dar es salaam

BODI ya Ligi Tanzania  (TPLB),imesisitiza  kuwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya mahasimu Yanga na Simba utapigwa Januari 4  mwakani.

Kabla ya bodi hiyo kutoa msimamo huo, kulikuwa na wasiwasi huenda mchezo huo utasogezwa mbele kutokana na mwingiliano wa ratiba ya ligi hiyo ya Kombe la Mapinduzi ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka mapema Januari, huku mwaka huu ikipangwa kuanza kutimua vumbi Desemba 30.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa bodi hiyo,  Stephen Mguto alisema;

“Tulichofanya sisi ni kuwasiliana na viongozi wa kamati ya maalum inayosimamia michuano ya Mapinduzi, ili watupe maoni yao kuhusu tariba ya ligi hapa Tanzania Bara.

“Tumeomba michuano ya Mapinduzi iwe ya  mtoano ili timu za huku ziweze kucheza mechi zake mara zitakapotoka, lakini kwa hao Simba na Yanga hata kama zitaingia hatua ya nusu fainali au robo zitatakiwa zirudi Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, hivyo hatutabadilisha ratiba mchezo huo,”alisema .

 Mguto alisema kwa kufanya hivyo itasaidia ratiba isibadilishwe mara kwa mara kwani itakabaki kama ilivyopangwa awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here