25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yamwita Mo mezani

pg32 agost 2Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya soka ya Simba, imemwita kwa majadiliano mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, kuhusu nia yake ya kutaka kuimiliki klabu hiyo kwa mfumo wa hisa.

Mfanyabiashara huyo jana aliwasilisha barua rasmi ya maombi kueleza nia yake ya kutaka kumiliki asilimia 51 za hisa, kwa kuweka Sh bilioni 20 katika klabu hiyo.

Simba kuonyesha kwamba wana nia ya kile alichokiomba Mo, wamemwandikia barua jana hiyo hiyo kumtaka kuhudhuria kikao cha kamati hiyo Agosti 15, mwaka huu ili kusikilizwa, kujadaliana na kupata mapendekezo ya mabadiliko hayo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Patrick Kahemele, alisema kwamba kamati hiyo ina nia na dhamira ya dhati juu ya lengo la Mo la kuomba umiliki wa hisa hizo.

“Uongozi upo tayari hata leo, lakini kuna taratibu lazima zifuatwe kabla ya kufikia hatua hiyo, ndio maana tumemwita katika kamati ili kujadiliana mambo muhimu ya kufanya,” alisema Kahemele.

Kahemele alisema kwamba baada ya wanachama na uongozi kukubaliana juu ya mabadiliko ndani ya klabu hiyo, walimwandikia barua Mo ya kutaka kuanza kushirikiana na kamati ya usajili inayoongozwa na Zacharia Hans Pope.

“Sekretarieti ya Simba imeagizwa na Kamati Tendaji kumwandikia barua Mo ya kumwomba awasiliane na Hans Pope au Katibu Mkuu Mtendaji ili waweze kushirikiana na kumaliza zoezi la usajili lililoanzishwa na kamati hiyo,” alisema Kahemele.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwasilisha barua rasmi katika klabu hiyo, Mo alisema kwamba ingekuwa vigumu kuiwasilisha barua hiyo kabla ya wanachama kukubali mabadiliko hayo.

“Jana nilimtuma mwakilishi wangu apeleke barua kwa uongozi wa klabu, ilikuwa na mchanganuo wa lengo langu la kutaka kumiliki hisa za asilimia 51 za klabu hiyo.

“Kabla ya hapo, kulikuwa na upotoshwaji mkubwa uliokuwa ukifanywa na viongozi wa klabu hiyo, lakini ijulikane tu kwamba nisingeweza kuwasilisha barua kabla ya wanachama kukubaliana na mfumo wenyewe,” alisema Mo.

Mo alisema akiwa katika harakati za kutangaza nia yake ya umiliki wa hisa hizo, alifanya mazungumzo na uongozi wa Simba akiwamo Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

“Viongozi wanaoongozwa na Aveva, hawana nia ya dhati ya mabadiliko, lakini tumechoka kuiendesha Simba kama inavyoendeshwa sasa.

“Kama uongozi ukikubaliana na mabadiliko hayo wakati tukisubiri mambo mengine yakamilike, nitakuwa tayari kuwasaidia katika usajili wa wachezaji bora wa kimataifa,” alisema Mo.

Pia alipendekeza wanachama wa klabu hiyo kupewa nafasi ya juu ya kumiliki miongoni mwa hisa zitakazotolewa na klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles