22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Simba yamuacha Manara, yamrejesha Kamwaga

Na Winfrida Mtoi

Uongozi wa Klabu ya Simba umeachana na Haji Manara na kumteua Ezekiel Kamwaga kuwa Kaimu wa Idara ya Habari na Mawasiliano kwa muda wa miezi miwili.

Hivi karibuni Manara aliingia katika mgogoro na uongozi wa klabu hiyo, akilalamikia  kutotendewa haki na kushutumiwa kuihujumu timu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo leo Julai 28, 2021, imeridhia matakwa ya Manara ya kutoendelea  kuhudumu katika nafasi ya usemaji wa klabu , hivyo kumshukuru kwa maneno aliyoyatumia kuwaaga Wanasimba.

“Bodi inamshukuru kwa maneno aliyoyatumia kuwaaga Wanasimba katika kundi la viongozi wa Simba (Simba HQ) na kwa kazi aliyoifanyia klabu katika kipindi alichishika nafasi hiyo na tunamtakia kila la kheri,” imesema taarifa hiyo.

Aidha bodi hiyo imesema Kamwaga  atashiriki katika  maboresho ya muundo na utendaji wa idara ya Habari na  baada ya  maboresho kukamilika, itatangaza fursa mbalimbali za ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles