30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Simba yajipanga kuiua Mbeya City

simba-sports-club-212-768x403NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba imeanza kuipigia hesabu Mbeya City wanayotarajia kucheza nayo Oktoba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, wekundu hao wamedai kuwa ili kuzoa pointi zote tatu wamepanga kufika mapema mkoani humo.

Wachezaji wa Simba ambao hawamo kwenye timu za Taifa, wanatarajia kuanza tena mazoezi leo baada ya mapumziko ya siku mbili, tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo muhimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Msimu uliopita Simba iliambulia patupu mbele ya Mbeya City, baada ya kufungwa mechi zote mbili walizocheza na timu hiyo, ilianza kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa kabla ya kulala 2-0 mkoani Mbeya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara, alisema wataondoka jijini hapa mapema kuelekea Mbeya ili kuzoea mazingira ya huko na kutimiza lengo lao la kulipa kisasi.

“Tunahitaji ushindi kwenye mchezo na Mbeya City hivyo tutahakikisha tunaupata na tumejipanga kwenda mapema kabisa mkoani humo na kujiandaa kikamilifu kuchukua pointi tatu,” alisema.

Manara alisema kwa upande wa wachezaji, wote wapo katika hali nzuri kimchezo na wataanza kufanya mazoezi yao katika Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi, Simba ilitakiwa kucheza na Ndanda katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona wikiendi iliyopita, lakini mchezo huo umepigwa kalenda ili kupisha maandalizi ya mchezo wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Malawi ‘The Flames’ utakaofanyika keshokutwa.

Simba hivi sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na jumla ya pointi 12, baada ya kucheza mechi tano, wakishinda nne African Sports (1-0), Mgambo Shooting (2-0), Kagera Sugar (3-1), Stand United (1-0) huku ikifungwa 2-0 na Yanga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,396FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles