24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Simba yaitengenezea hesabu kali Mwadui

Theresia Gasper-Dar es Salaam

KIKOSI cha Simba, kinatarajia kuingia kambini leo kuendelea na maandalizi, kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho(ASFC) dhidi ya Mwadui, unaotarajiwa kuchezwa Januari 26 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Simba ilirejea Dar es Salaam yaliko makao yake makuu Jumatatu wiki hii ikitokea Mwanza, ilikochezaa michezo miwili ya  Ligi Kuu Tanzania Bara, ikianza kuivaa Mbao FC na kushinda mabao 2-1 kabla ya kuitungua Alliance mabao  4-1, michezo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Wekundu hao jana waliendelea  na mazoezi kwenyea uwanja wao wa Mo Simba Arena  jijini hapa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema wanaendelea na mazoezi ili kujiweka fiti kabla ya kuivaa Mwadui.

“Baada ya kurejea kutoka Mwanza tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku moja na leo (jana) tumeendelea na mazoezi lakini kesho (leo) tunatarajia kuingia kambini kuendelea na maandalizi ya mwisho,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles