Theresia Gasper-Dar es Salaam
KIKOSI cha Simba, kinatarajia kuingia kambini leo kuendelea na maandalizi, kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho(ASFC) dhidi ya Mwadui, unaotarajiwa kuchezwa Januari 26 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Simba ilirejea Dar es Salaam yaliko makao yake makuu Jumatatu wiki hii ikitokea Mwanza, ilikochezaa michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ikianza kuivaa Mbao FC na kushinda mabao 2-1 kabla ya kuitungua Alliance mabao 4-1, michezo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Wekundu hao jana waliendelea na mazoezi kwenyea uwanja wao wa Mo Simba Arena jijini hapa.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema wanaendelea na mazoezi ili kujiweka fiti kabla ya kuivaa Mwadui.
“Baada ya kurejea kutoka Mwanza tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku moja na leo (jana) tumeendelea na mazoezi lakini kesho (leo) tunatarajia kuingia kambini kuendelea na maandalizi ya mwisho,” alisema.