27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaiomba TFF kurejea Taifa

patrick-kahemeleNa ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba, umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhama Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na  kurejea  Uwanja wa Taifa kutokana na  sababu mbalimbali, ikiwamo usalama wa afya za wachezaji.

Uamuzi wa Simba unakuja huku wakiwa tayari  wameutumia uwanja huo  kucheza michezo mitatu  ya  Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kufanyiwa maboresho yaliyogharimu Sh bilioni 12 za Tanzania.

Taarifa iliyotumwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Patrick Kahemele, ilieleza kuwa usalama wa afya za wachezaji wao upo hatarini kutokana na plastiki za kushika nyasi bandia za uwanja huo  kukauka,  hivyo kuhatarisha afya za wachezaji wanaotumia.

“Kuna haja ya kuufanyia marekebisho uwanja  huo kwa kuweka plastiki mpya kutokana na zile zilizopo zilikaa kwa miaka kadhaa bila ya kutumika wakati uwanja ulipokuwa umefungwa kwa maboresho.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam FC uliochezwa hivi karibuni, tumepokea malalamiko pia kutoka kwa mashabiki ambao wamedai walishindwa kuingia uwanjani  kutokana na msongamano, hali hiyo inatokana na  ongezeko la watu jijini Dar es Salaam  na kuongeza mashabiki wanaohitaji kuingia uwanjani,” alisema Kahemele.

Mbali na  ombi hilo, Kahemele alitoa wazo la kuwapo kwa mchezo wa kujaribu matumizi ya mfumo wa  tiketi za elekroniki, ambalo alipendekeza kufanyika kwa siku tatu,  kesho, Alhamisi  na Ijumaa.

“Majaribio hayo yatatufanya  tutumie vema  mfumo huo  katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Majimaji kabla ya mchezo wa watani wetu wa jadi  timu ya  Yanga,  kwani  bila kujaribu kunaweza kuwa na madhara,” alisema Kamehele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles