23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Simba yafanya kweli yaizima Mashujaa

Mwandishi wetu , Kigoma

TIMU ya Simba jana  ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0  dhidi ya Mashujaa katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika  mkoani Kigoma.

Ushindi ni wa pili kwa Simba katika mchezo wa kirafiki baada ya Jumamosi iliyopita kuibuka na matokeo  kama hayo  dhidi ya Bandari  ya Kenya, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa jana bao pekee la Simba lilifungwa  dakika ya 56 na kiungo wa timu hiyo, Sharaf Shiboub ambaye aliunganisha  kwa kichwa krosi ya  Said Ndemla.

 Kipindi cha kwanza timu hizo  zilionekana kushambuliana kwa zamu huko kila moja ikihitaji kupata bao la kuongoza, lakini milango ilikuwa migumu kufunguka.

 Mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi,  Kocha wa Simba, Patrick Aussems  alifanya mabadiliko kwa kumtoa Francis Kahata na nafasi yake kuchukuliwa na Shiboub na kupeleka kilio kwa  Mashujaa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. 

Simba wanatarajia kushuka dimbani kesho kucheza na mabingwa wa Burundi Aigle Noir,  ukiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

Wekundu wa Msimbazi wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, utakaochezwa kuchezwa Oktoba 23 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles