24.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 24, 2021

SIMBA YABANWA IKIKABIDHIWA UBINGWA

MWAANDISHI WETU

TIMU ya Simba imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa suluhu  na Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi ukiambatana na sherehe za Wekundu hao wa Msimbazi kukabidhiwa ubingwa.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo za kuikabidhi Simba taji hilo la tatu mfululizo ziliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangwala, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas na Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.

Wakati Simba ikikabidhiwa ubingwa huo, huku ikishindwa kupata ushindi mchezo wa tatu mfululizo, watani zao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Bao pekee lililoipa Yanga pointi tatu lilifungwa na kiungo wake, Bernard Morrison dakika ya 78 ya mchezo huo.

Ushindi huo unaifanikiwa Yanga kuendeleza ubabe dhidi ya Kagera, ikiwa ni siku nane zimepita tangu walipoichapa mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Juni 30, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  

Morrison ni kama ametuma salamu kwa Simba kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba sasa imecheza michezo dakika 270 za ligi bila kufunga bao, ikianza kulazimishwa suluhu na Tanzania Prisons, kisha kupata matokeo kama hayo dhidi ya Ndanda na Namungo.

Timu hiyo imejikusanyia pointi 81 baada ya kucheza michezo 34, ikishinda 25, sare sita na kupoteza mitatu.

Simba ilianza mchezo huo kwa kumiliki mpira na kucheza pasi nyingi hasa eneo la katikati ya uwanja.

Namungo kwa upande wao, walianza kwa kasi ya kusukuma mashambulizi kwenye lango la Simba  wakioneka wazi wamepania kuibuka na ushindi.

Dakika ya tatu ya, Bigirimana Blaise alijarajibu kuifungia Namungo bao la kuongoza kwa shuti kali lakini mpira uliokolewa na  mlinda malngo wa Simba, Beno Kankolanya.

Dakika ya  21, Meddie Kagere alipiga shuti kali langoni mwa Namungo, lakini kipa wa  timu hiyo, Nurdin Barola alimama imara na kuondosha hatari hiyo.

Dakika ya 32, Lucas Kikoti aliwatoka mabeki wa Simba na kupiga shuti kali linalotua mikononi mwa Kakolanya.

Dakika ya 33, Kikoti alilimwa kadi ya njano kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa mwamuzi.

Kipindi cha pili kilimalizika kwa timu hizo kwenda mapumziko bila kufungana,kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko ya kumtoa Mohammed Hussein na kuingia Shiza Kichuya.

Namungo ilingia kipindi cha pili kama mbogo aliyejeruhiwa  ikionekana kulisakama lango la Simba kama nyuki.

Dakika ya 48, beki wa Simba alitolewa nje baada ya kuumia goti, huku nafasi yake ikichukuliwa na Gadiel Michael.

Dakika ya 63,Deo  Kanda aliingia kuchukua nafasi ya Francis Kahata katika kikosi cha Simba

Dakika ya 66, Miraji Athuman aliwalima chenga walinzi kadhaa wa Namungo, hata hivyo shuti alilopiga lilikwenda nje ya lango.

Dakika ya 71, Simba ilifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Ibrahim Ajib na nafasi yake kuchukuliwa na Cyprian Kipenye.

Dakika ya 88, nusura Namungo ijipatia bao, lakini  mpira wa kichwa uliopigwa na Kikoti unagonga nguzo kabla ya kuokolewa na walinzi wa Simba.

Hadi dakika 90 za mchezo huo zinakamilika, timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa hazijafungana

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,966FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles