26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Simba waua ng’ombe 20

Malima Lubasha- Serengeti

KUNDI la wanyama aina ya simba kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) mkoani Mara, wamevamia zizi la mkazi wa Kijiji cha Robanda, Samwel Mahewa na kuua ng’ombe 20, huku wengine 8 wakipotea.

Ng’ombe wote wameelezwa kuwa na thamani ya Sh milioni 15.4.

Tukio la kuuawa ng’ombe hao, lilitokea Novemba 3, mwaka huu saa 7.00 usiku katika  Kitongo cha Momorogoro kila ng’ombe mmoja akithaminishwa kwa thamani ya Sh 550,000.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki,  Mahewa alisema simba walivamia zizi lake na kuua ng’ombe 17 hapo hapo na kujeruhi wengine watatu ambao walikufa baadaye.

Alisema ng’ombe 8 walikimbia kutoka ndani ya zizi mpaka sasa hawajafamika waliko, licha ya  juhudi kubwa za kuwatafuta bila mafanikio.

Alisema ndani ya zizi kulikuwa na ng’ombe ambao baadhi ni wazee na wengine walikuwa hawaoni, lakini jambo la ajabu simba hawakuwaua, bali walikuwa wanaua na kula wale walionona.

“ Nimepata hasara kubwa,ng’ombe hawa nilikuwa nawategemea katika kilimo,sijui nitaanzaje maisha haya,”alisema.

Ofisa Maliasiili Wanyamapori Wilaya ya Serengeti, John ole Lendoyani alithibitisha kuuawa ng’ombe hao na kumtaka Mahewa kujaza fomu ya kifuta machozi.

Alisema mchakato ukikamilika atalipwa kifuta machozi cha Sh 50,000 kwa kila ng’ombe na kutoa wito kuimarishwa ulinzi na kujenga mazizi imara.

Wakati huo huo usiku wa kuamkia Novemba 16, mwaka huu saa 2.00 usiku katika Kijiji cha Nyichoka,kundi la simba kutoka Hifadhi ya Serengeti walivamia zizi la Samwel Makena na kuua ng’ombe mawili na kujeruhi wengine.

Wananchi waliokuwa doria walifanikwa kuwafukuza kabla ya kuleta madhara zaidi ya kuua mifugo kaya jirani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles