24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Simba wataka Yanga waje wamalizane

5Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM
UONGOZI wa timu ya Simba, umesema upo tayari kukaa na Yanga meza moja kumaliza mgogoro uliopo baina yao na watani wao hao wa jadi juu ya beki wao, Hassan Ramadhani ‘Kessy’.

Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), juzi ilikaa kikao cha kuamua hatima ya mchezaji huyo na kutoa saa 72 kwa viongozi wa Yanga kumalizana na Simba.
Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jana licha ya agizo hilo la kamati, Yanga wamekaa kimya jambo alilosema si la kistaarabu.

“Sisi kama Simba hatuoni sababu ya kuendelea na malumbano haya na kumnyima  haki  Kessy, lakini wenzetu wanapaswa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa, sasa wamekataa kukaa meza moja tuyazungumze,” alisema.

Kaburu aliongeza imekuwa kawaida kwa Yanga kuchukua wachezaji kutoka Simba, lakini kwa suala hili wanapaswa kujifunza kuwa wastaarabu na kwamba wangezungumza ili mambo yamalizike na mchezaji huyo awe huru.

Akizungumza na MTANZANIA juu ya suala hilo Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema lipo juu ya kamati na kudai kuwa baada ya saa hizo kupita watatoa maamuzi.

“Siwezi kusema tumezungumza au la, lakini kila kitu kitajulikana baada ya hizo saa 72, nasisitiza kuwa suala hili ni la kamati na si vinginevyo,” alisema katibu huyo.

Yanga na Simba zimeingia kwenye mzozo juu ya usajili wa beki Kessy ambaye anadaiwa kusaini Yanga akiwa bado anatumikia adhabu ya kusimamishwa mechi tano na timu yake ya Simba.

Kessy alipewa adhabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kugundulika kuwa na utovu wa nidhamu, adhabu ambayo inadaiwa  hakuimaliza na kuamua kusaini mkataba mpya na timu ya Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles