30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Simba wana nafasi, lakini soka lina matokeo ya kikatili

MAREGES NYAMAKA-DAR ES SALAAM      

SIMBA  wamekuwa na mwanzo mzuri wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika(Caf), baada ya katikati ya wiki iliyopita kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows ya Eswatin zamani Swaziland.

Ni kama walivyowahi kufanya hivyo huko nyuma, ikiwamo Februari 17, 2008 walipofanikiwa kuwafunga mabao 3-0 Awassa ya Ethiopia, ulikuwa ni ushindi mkubwa kweli kweli katika matumizi mazuri ya Uwanja wa nyumbani.

Katika mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Awassa Kenema na  kulimalizika kwa sare 1-1 ilikuwa faida kwa Simba kuendea hatua inayofauta, kwa faida ya mabao mengi waliovuna mechi ya awali nyumbani.

Hiyo inaweza kuwa kumbukumbu nzuri kuanzia kwa mashabiki, uongozi hadi wachezaji wenyewewe wa Simba ambao  kesho wanatarajia kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows kusaka teketi ya kusonga mbele.

Mabingwa hao Ligi Kuu Tanzania Bara wanashuka dimbani hapo wakiwa na faida hiyo ua mabao mengi, huku milima mrefu wa kupanda wakiwa nao wenyeji wao.

Hata hivyo katika soka bado Mbabane wana nafasi ya kupindua matokeo na kusonga mbele iwapo tu Simba watafanya makosa kama ambavyo anaamini kocha wa Waswatini hao, Kinnar Phir.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems pia akiwasisitiza wachezaji wake kwamba bdo dakia nyingine 90 mbichi kabisa wakiitaji kupambana kupata matokeo bora ili kusonga hatua inayofuata.

Uwepo wa wachezaji wengi wazoefu na michuano ya Kimataifa ni silaha kubwa kwa Mbeligiji huyo. Miongoni mwa nyota hao ni straika, Medie Kagere aliyefunga bao la tatu baada ya makosa yaliyofanywa na kipa.

Kagere anajukina umahiri wake tangu akiwa na kikosi cha Gor Mahia kilichofika hatua ya makundi msimu uliyopita.Clatous Chama, achilia kufunga kwake bao kali la nne mchezo.

Lakini  pia kupewa nafasi ya nahodha msaidizi katika timu ya Taifa ya Zambia ana kitu cha tofauti, yeye ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.

Pascal Serge Wawa amekuwa ‘kamanda’ katika eneo la ulinzi tangu akiwa timu ya El Merrehk ya Sudan, Emmanuel Okwi, John Bocco, Erasto Nyoni na Aishi Manula.

Pamoja na Simba kuwa na rekodi nzuri ya michuano ya Kimataifa ikiwamo hiyo ya  Ligi ya Mabingwa ,ingawa hawajawahi kutwaa taji hilo, miaka ya karibuni wamekumbana ugumu maradufu.

Simba mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa  na kujikuta wanatolewa hatua za awali kabisa ilikuwa ni  Februari 17, 2013 walipokubali kichapo cha bao jumla ya mabao 5-0.

Hatua hiyo ilitokana na kufungwa bao 1-0 Uwanja wa nyumbani, Taifa kabla ya mvua nyingine ya mabao 4-0 ugenini. Ni somo kwa tosha katika twira hiyo.

Lakini kama hiyo haitoshi  msimu uliyopita walioshiriki Kombe la Shirikisho, mabao mawili waliyoruhusu ardhi ya nyumbani katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Al Masry kilikuwa kitanzi kwao, kwani hata suluhu waliopata mchezo wa marudiano iliwabeba wapinzani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,688FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles