26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Simba wajipanga upya sakata la Kessy

kessy

NA ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KLABU ya soka ya Simba inajipanga kuhakikisha inaongeza wajumbe kwenye kikao cha kujadili sakata la beki wake wa zamani, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, baada ya kushindwa kufikia mwafaka Jumapili iliyopita.

Katika kikao kilichopita, klabu hizo ziliwakilishwa na makatibu wakuu ambapo kwa upande wa Simba alikuwa ni Patrick Kahemele na Yanga ni Baraka Deusdedit.

Inadaiwa kuwa Wekundu hao wa Msimbazi wanafanya mipango ya kuhakikisha wanasheria, Damas Ndumbaro na Evodius Mtawala wanaingia kwenye kikao kinachofuata ili kujadili suala hilo.

Chanzo cha habari za uhakika zilizolifikia MTANZANIA jana, kimeeleza kuwa suala hilo bado halijatolewa uamuzi wa mwisho lakini linaendelea kufanyiwa kazi.

Katika sakata hilo, Kessy anadaiwa kukiuka kanuni za usajili baada ya kusaini mkataba wa kuichezea Yanga, huku akiwa bado ana mkataba na klabu yake ya zamani ya Simba.

Akizungumzia suala hilo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema katika kikao kilichopita kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliutaka uongozi wa Simba kuwasilisha vithibitisho vya mkataba wa beki huyo ili kujiridhisha.

“Kamati pia inahitaji kumbukumbu za malipo ya mshahara wa mchezaji huyo kwa miezi mitatu kabla ya kujiunga na Yanga,” alisema Lucas.

Katika hatua nyingine, TFF imewataka wachezaji wote wenye mikataba ambao wanacheza Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), kuwasilisha nakala za mikataba yao ili ziwasaidie wanapokuwa na migogoro na klabu zao.

TFF imefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka klabu zinazoshiriki ligi mbalimbali zikidai wachezaji wamekiuka mikataba yao.

Alisema wachezaji wanapaswa kuwa na nakala tatu ikiwamo ya klabu inayomsajili, TFF na yake ili kujilinda watakapopata matatizo kwenye klabu zao.

“Wachezaji wengi hawajawasilisha nakala za mikataba yao TFF, wanasubiri wapate matatizo ndiyo wakumbuke kufanya utaratibu huo,” alisema Lucas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles