27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga Vs Simba zitakavyomwonyesha Rais Caf ulimwengu mwingine leo

Na WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

POPOTE utapopita katika vijiwe vya soka, mazungumzo yaliyotawala ni kuhusu mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yanga.

Timu hizo zinatarajia kushuka dimbani leo kuumana, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara umekuwa na mvuto wa aina yake kutokana na hali ya vikosi vyote viwili.

Timu hizo zilipokutana mzunguko wa kwanza mchezo ulichezwa Januari 4 mwaka huu kwenye uwanja huo, dakika 90 zilikamilika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.

Matokeo hayo yaliwafanya wadau wa timu hizo kutamani siku ya mchezo wa marudiano ifike haraka na hatimaye imefika hii leo.

Mwenyeji wa mchezo wa leo ni Yanga.

Mchezo huo umeongezewa mvuto kutokana ugeni kutoka Shirikisho la Soka Afrika(Caf). Ugeni huo si mwingine bali ni wa Rais wa Caf, Ahmad Ahmad.

Lakini pia vikosi vya timu hizo safari hii vitakuwa na maboresho, baada ya klabu hizo mbili kufanya usajili wakati wa dirisha  dogo. 

Yanga ndiyo iliyofanya usajili mkubwa na kikosi chake kubadilika zaidi.

Lakini nyota wawili kutoka katika timu hizo, Luis Miquissone wa Simba na Bernard Morrison kwa Yanga ndiyo wanaotawala majadiliano ya wadau wa soka.

Ukiachana na nyota hawa  wawili ambao wanatarajiwa kushuka burudani ya maana kutokana na kipaji alichojaliwa kila mmoja, vipo vitu vingi vinavyotarajiwa kujitokeza katika mchezo huo  na kumstaajabisha Rais wa Caf, Ahmad na kuondoka na faili lililojaa.

Naamini kuna vitu vingi ambavyo Rais huyo, hajawahi kuvishuhudia katika michezo mingi ya wapinzani‘derby’aliyowahi kupata nafasi ya kushuhudia.

Pamoja na Ahmad kuwa na ziara ya kimichezo hapa nchini, lakini moja ya vitu vilivyomleta ni kushudia mcheza huo baada ya kushangazwa na idadi kubwa ya mshabiki katika mechi iliyopita.

Kutokana na hilo, mashabiki wanatakiwa kutumia fursa hiyo kujitangaza na kuweka utulivu wa hali ya juu ili wapewe hadhi ya tofauti Afrika.

Baadhi ya vitu ambavyo ni kivutia katika mchezo wa leo na vitamfanya Ahmad Ahmad, ajihisi yupo katika ulimwengu mwingine na kuondoka na vitu vingi vya kufanyia kazi;

Vioja

Ni jambo lililowazi kuwa mashabiki wa timu hizo mbili kongwe hapa nchini, wamejizolea sifa ndani na nje ya nchi kutokana na vibwanga vyao uwanjani siku timu zao zinapocheza.

Kitendo hicho kimekuwa kivutio kikubwa katika mechi mbalimbali, lakini zaidi wanapokutana wenyewe kwa wenyewe  kutokana na utani na kejeli nyingi wanazotupiana.

Kama ni mara yako ya kwanza kuwaona mashabiki hao unaweza kusema ni maadui wa muda mrefu, lakini kumbe  tambo hizo zinamalizwa na dakika 90 na wanapotoka hapo ni marafiki. 

Hali hiyo atakapoishuhudia Ahmad, atajihisi kabisa yupo katika ulimwengu mwingine na hata kutamani kuendelea kushuhudia burudani hizo.

Viongozi wa nchi kupishana na jezi

Kitu kingine chenye mvuto katika mchezo wa Simba na Yanga ni kitendo cha baadhi ya viongozi wa nchi kuweka majukumu na suti zao pembeni na kutinga jezi za timu, kisha kuelekeza akiri katika mpambano huo.

Si kila nchi ambayo unaweza kukutana na viongozi wakubwa wa serikali wakishangilia timu zao kwa mzuka wa hali ya juu, hali inayoongeza msisimko wa soka.

Kwa kawaida katika mechi hizo shida zotem vyeo vinawekwa pembeni na watu kuwa kitu kimoja, kuangalia nini kitazaliwa ndani ya dakika 90.

Siku ya nyekundu, nyeupe, njano, kijani

Rangi nne yaani nyekundu na nyeupe ambazo ni utambulisho wa Simba na njano na kijani zinazoitambulisha Yanga zitapendezesha Jiji la Dar es Salaam leo.

Ahamad  ataanza kupata viashiria vya nini kinaendela kuanzia barabarani atakakokuwa anapita.

Atakapofika uwanjani sasa ndipo naye atatamani kupewa jezi kwa sababu kila takapochungulia rangi zilizotawala ni hizo, huku kukiwa na amsha amsha nyingi kila upande ukipiga kelele.

Tochi za simu

Hii ni staili ya kizazi kipya ya ushangiliaji iliyochangiwa na ukuaji wa teknolijia na matumizi ya simu za mkononi kuongezeka.

Kuna wakati kila shabiki uwanjani hapo uwasha tochi ya simu yake ikiwa ni namna mojawapo ya kuhamasisha.

Mara nyingi inatokea muda ambao  mechi imepamba moto na kuna timu tayari imeshafungwa, hivyo mashabiki hutumia simu kuongeza ushangiliaji.

Mchuano nyota wazawa na wageni

Mchezo wa Simba na Yanga moja ya mechi inayowapa majina wachezaji au kuyaharibu kutokana na vile watakavyocheza, hali hiyo inaongeza umakini na kuwafanya wacheze kwa kiwango chao chote.

Kutokana na hilo mchuano unakuwa mkali kati ya wachezaji wazawa na wale wakigeni, kila mmoja akisaka heshima mbele ya umati mkubwa wa mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles