24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 23, 2023

Contact us: [email protected]

Simba SC kuifuata UD Songo kibabe

Theresia Gasper -Dar es salaam

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wanatarajia kuondoka leo kuifuata UD Songo, kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa kesho nchini Msumbiji.

Simba wataondoka wakiwa na wachezaji 19 huku kocha wao, Patrick Aussems akitamba kuumaliza mchezo mapema kabla ya marudiano ambao utafanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Huo utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Wekundu wa Msimbazi huku wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23, 24 na 25 mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems alisema kikosi chake kimejiandaa vizuri na mchezo huo huku wachezaji watatu wakiwa bado hawajaanza mazoezi sababu ya majeruhi, nyota hao ni Aishi Manula, Ibrahim Ajib na Wilker Henrique.

“Tumefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo muhimu kwetu, wachezaji wapo katika hali nzuri kasoro watatu ambao ni majeruhi.

“Tunawajua wapinzani wetu, tulianza kuwafuatilia tangu ratiba ilipotoka, tunajua timu yao imebadilika kwa kiasi kikubwa, tumejipanga vizuri dhidi yao,” alisema.

Kikosi hicho kiliweka kambi ya wiki mbili nchini Afrika Kusini kujiandaa na  michuano hiyo ikiwa pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Msimu uliopita, Simba waliishia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo, baada ya kutolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini msimu huu wamepania kufanya vizuri zaidi ikiwezekana kutwaa taji hilo kubwa barani Afrika kwa upande wa klabu.

“Malengo yetu ni kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita, hatuhitaji kuishia hatua za awali, kwa usajili tuliofanya tunaweza kufika mbali zaidi,” aliongeza Mbelgiji huyo.

Itakumbukwa kuwa UD Songo walitolewa hatua za awali msimu uliopita na Nkana FC ya Zambia, ambao walicheza dhidi ya Simba na Wekundu wa Msimbazi kutinga hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 4-3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles