24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Simba sc chalii

Pg 32*Toto yaipiga moja na kuipunguzia kasi ya ubingwa

*Mashabiki Simba, Yanga wapigwa mabomu Taifa

NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Simba jana ilipunguzwa kasi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu na kushindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Toto Africans.

Kwa matokeo ya jana Simba ilishindwa kutamba katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kukosa pointi tatu muhimu ambao zingewashusha kileleni watani wao wa jadi, Yanga wanaoongoza kwa pointi 59.

Wekundu hao wa Msimbazi wamebaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa kujisanyia pointi 57 baada ya kucheza michezo 25, wakifuatiwa na Azam FC nafasi ya tatu kutokana na pointi 55 walizonazo baada ya kushuka dimbani mara 24.

Simba waliingia uwanjani wakiwa na shauku ya kupata bao la mapema ili waweze kukamata usukani, lakini mipango yao ilianza kutibuliwa baada ya Toto kuandika bao pekee la ushindi dakika ya 19 kupitia kwa mshambuliaji wake, Waziri Junior.

Junior alifunga bao hilo baada ya kuachia shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari baada ya kunasa mpira uliookolewa na mchezaji wa Simba, Novaty Lufunga.

Wakati Simba ikiendelea kupambana kutafuta nafasi ya kusawazisha bao hilo, mwamuzi, Ahmada Simba, kutoka Kagera, alimuonyesha kadi nyekundu na kumtoa nje ya uwanja kocha wa timu hiyo Mganda, Jackson Mayanja, kwa kumtolea maneno ya kuudhi.

Dakika ya 27, Awadhi Juma, aliikosesha timu yake bao la wazi baada ya kushindwa kuunganisha vyema kwa kichwa mpira wa krosi ndefu iliyochongwa na Daniel Lyanga.

Baada ya Mayanja kutolewa, kocha wa makipa wa timu hiyo, Adam Abdallah, alilazimika kubeba majukumu ya kuliongoza benchi la ufundi kutokana na kukosekana kwa kocha msaidizi ndani ya kikosi hicho.

Hadi mapumziko Simba walikuwa nyuma kwa bao moja, ambapo walianza kipindi cha pili kwa kupata pigo jingine baada ya beki, Hassan Ramadhani ‘Kessy’ kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 46 baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Toto, Edward Christopher.

Timu hizo ambazo zilikuwa zimekamiana kwa dakika zote za mchezo, ziliendelea kupambana kwa kasi uwanjani kwa kila mmoja kushambulia lango la mpinzani wake lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwa pande zote.

Baada ya mchezo kumalizika, polisi waliokuwepo uwanjani walilazimika kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisubiri kulipiga mawe basi la wachezaji.

Mashabiki wa Yanga nao walipigwa mabomu ya machozi na askari hao baada ya kulizonga basi la Toto wakishinikiza lizimwe ili walisukume ili kulitoa nje ya uwanja.

Simba: Vicent Angban, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Mohamed Hussein, Novaty Lufunga, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Peter Mwalyanzi/Ibrahim Ajibu, Awadhi Juma, Daniel Lyanga, Hamis Kiiza na Mussa Hassan ‘Mgosi’.

Toto: Musa Kirungi, Erick Mlilo, Salum  Chukwu, Yussuf  Mlipili, Hassan Khatib, Carlos Protas, Jama Soudy/Salmin Hozza, Abdallah Seseme, Waziri Junior, Edward Christopher na Jafari Mohamed/William Kimanzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles