22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Simba nusura wamchape Micho Sauzi

Mohamed Kassara

TIMU ya Simba imefunga ziara yake ya michezo ya kirafiki Afrika Kusini, kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Orlando Pirates katika mchezo uliochezwa jana Uwanja wa Rand.jijini Johanesburg.

Simba ilianza kujipatia bao kupitia kwa kuingo, Clatous Chama  dakika ya 33, lakini Augustine Mulenga aliisawazishia Pirates dakika ya 40.

Pirates inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Sredojević  ‘Micho’, aliyeifundisha timu hiyo ya Jangwani mwaka 2007.

Sare hiyo ni ya pili mfululizo, baada ya kucungana bao 1-1 na Township Rollers inayoshiriki Ligi Kuu Botswana.

Pia iliichapa Orbet TVET mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza, kabla ya kuitandika timu ya Ligi Daraja la Kwanza ya Platinum Stars mabao 4-1 katika mchezo wa pili.

Baada ya mchezo, kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kinatarajia kurejea nchini kesho,  kwa ajili ya kilele cha siku ya  klabu hiyo  maarufu ‘ Simba Day’ ambacho kitafanyika Agosti 6, kwa kuivaa Power Dynamos ya Zambia

Simba inakabiliwa na kibarua kizito cha kusafiri hadi nchini Msumbiji, ambako itaumana na UD Songo, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utachezwa kati ya Agosti 8 na  11, huku mchezo wa marudiano ukipangwa kupigwa kati ya Agosti 23 na 25, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi waliweka kambi kwenye hoteli ya Royal Marang iliyoko Mji wa Rustenburg na kutumia Uwanja wa Bafoken Sports Campus kujifua kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa.

Simba imetumia michezo hiyo kupima kikosi chake na kuwaunganisha  wachezaji wapya na wale waliokuwepo ili kujenga kikosi imara  kitakaochokuwa na shughuli pevu ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo imejiwekea malengo ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo msimu huu, baada ya kuishia robo fainali msimu uliopita kwa kutolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) kwa jumla ya mabao 4-1.

Katika kuhakikisha inatimiza azma hiyo, Simba  imesajili wachezaji wapya 11, sita wakiwa wa kigeni ambao ni Deo Kanda(DRC), Francis Kahata (Kenya), Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Vieira na Henrique Wilker da Silva (Brazil) na Sharaf Eldin Shiboub (Sudan).

Wazawa ni, Ibrahim Ajib, Beno Kakolanya na Gadiel Michael wote kutoka Yanga, wengini ni Miraji Athuman(Lipuli) na Kennedy Juma (Singida United).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles