30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Simba ni dozi tu

Theresia Gasper- Dar es salaam

KIKOSI cha Simba kinatarajia kuendelea na mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi hicho kilipewa mapumziko ya siku moja jana na leo wataendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gymkhana, jijini hapa.

Wekundu wa Msimbazi hao, katika mchezo wa kwanza, walitoka suluhu dhidi ya UD Songo, nchini Msumbiji.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Kesho (leo) mchana tutaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gymkhana kujiweka fiti.

“Tunakabiliwa na mchezo mgumu mbele yetu na mipango yetu ni kupata pointi tatu muhimu.”

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, alisema kuwa kikosi chake kinazidi kuimarika hivyo anaamini watapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Alisema amepata kile anachokihitaji kupitia mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam walioshinda kwa mabao 4-2 kwenye Uwanja wa Taifa wikiendi iliyopita.

 “Kwa muda huu uliobakia, nitaendelea kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu ili tufanye vizuri kwenye mechi zetu, ukizingatia tutakuwa nyumbani,” alisema.

Wekundu wa Msimbazi hao wamepania kufanya kweli msimu huu ambao baada ya kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii, kwa sasa wanaelekeza nguvu zao michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles