23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

SIMBA NGUVU ZOTE KWA AL MASRY

  • Ni baada ya kulazimishwa sara ya 3 – 3 na Stand United

NA MOHAMED KASARA-DAR ES SALAAM

BAADA ya kubanwa mbavu na Stand United, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema wanasahau yaliyopita na kuelekeza akili zao katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri.

Simba jana ililazimishwa sare ya mabao 3-3 na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo, ilishindwa kulinda mabao yake kila ilipopachika wavuni hivyo kuifanya Stand United kuchomoa.

Kwa matokeo hayo, Simba imesalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 46 baada ya kucheza michezo 20, ikitengeneza pengo la pointi sita na hasimu wake Yanga ambayo ipo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 40, lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika, Djuma, alisema jana ilikuwa siku mbaya kwao kutokana na Stand United kusawazisha kila bao walilofunga katika mchezo huo.

“Leo ni siku mbaya kwetu na hii huwa inatokea katika soka, kama unavyojua tunacheza mechi nyingi katika kipindi kifupi, inaweza kuwa uchovu au wapinzani wetu walijipanga vizuri, lakini lengo letu lilikuwa kushinda, tunaachana na yaliyopita tunaangalia mchezo wetu ujao,” alisema Djuma.

Djuma alizungumzia kukosekana kwa mastraika wake wawili tegemeo, Emmanuel Okwi na John Bocco, katika mchezo wa jana akisema wachezaji hao hawakuwa fiti kwa mchezo huo.

“Hatujawatumia Okwi na Bocco kwa sababu hawako fiti, lakini si kwa ajili ya mchezo na Al Masry, sisi tunaangalia ligi kwanza, unaweza usimtumie Okwi kwa makusudi leo alafu kesho akaumia akakaa nje muda mrefu itakuwa na faida gani sasa,” alisema.

Dakika ya sita, Kwasi aliifungia Simba bao la kuongoza baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Stand United, Mohamed Makaka, aliyepangua kiki ya Laudit Mavugo.

Dakika ya 18, mwamuzi Frolentino Zabron, alimlima kadi ya njano Birigimana Blaise, baada ya kumfanyia madhambi Mzamiru Yasin.

Dakika ya 19, mkwaju wa Mavugo ulitoka nje kidogo ya lango la Stand United.

Dakika ya 22, Mavugo alirekebisha makosa yake baada ya kuifungia Simba bao la pili baada ya kuunganisha wavuni krosi ya Shomari Kapombe.

Dakika ya 27, kiki ya Vitalis Mayanga, iliwababatiza mabeki wa Simba na kuwa kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.

Dakika ya 31, Tariq Seif, alikunjuka na kuachia fataki ambalo lilitoka nje kidogo ya lango la Simba.

Dakika ya 35, Tariq aliwainua wapenzi wa Stand United baada ya kuifungia timu hiyo bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya Blaise.

Dakika ya 38, beki Ally Ally wa Stand United, alilimwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Mavugo.

Dakika ya 40, Aron Lulambo, aliisawazishia Stand United kwa kuifungia bao la pili baada ya kona aliyoichonga kutinga moja kwa moja wavuni.

Dakika ya 43, Ndikumana Selemani, alilimwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi, Erasto Nyoni.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa timu hizo kufungana  mabao 2-2.

Kipindi cha pili kilipoanza, kocha wa Simba, Pierre Lechantre, alifanya mabadiliko akimtoa Mavugo na kumwingiza Juma Liuzio.

Dakika ya 56, Kichuya akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga alipiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa wa Stand United, Mohamed  Makaka.

Dakika ya 59, Nicholaus Gyan, aliwainua mashabiki wa Simba baada ya kuifungia timu yake hiyo bao la tatu baada ya mabeki wa Stand United kuchelewa kuondosha mpira wa kona iliyochongwa na Mzamiru uliokuwa ukizagaa langoni mwao.

Inaendelea………………. Jipatie gazeti lako #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles