33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Simba Moto, Ruvu Shooting moto

Theresia Gasper -Dar es salaa

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti, huku Ruvu Shooting ikimkaribisha bingwa mtetezi Simba, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mchezo mwingine utakuwa kati ya Azam FC, ambayo watakuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba,  Mwanza.

Biashara United  itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar  dimba la Karume, Musoma.

Simba itakutana na Ruvu Shooting ikiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons, katika mchezo wake uliopita uliochezwa dimba la Uhuru.

Wapinzani wao Ruvu Shooting watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupata kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Namungo FC, Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Wekundu hao wa Msimbazi, Simba ina inashika uogozi kwenye kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa imejikusanyia pointi 22, baada ya kushuka dimbani mara tisa, ikishinda michezo saba, sare moja na kupoteza mmoja.

Ruvu Shooting inashika nafasi ya nane, ikiwa imejikusanyia pointi 15, sawa na Mtibwa Sugar pamoja na JKT Tanzania, zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita, Simba ilishinda mabao 5-0, mchezo wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kushinda mabao 2-0, mchezo wa mzunguko wa pili uwanja huo huo.

Kurejea  Simba kwa wachezaji Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Miraji Athuman waliokuwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na  Meddie Kagere aliyekuwa kikosi cha Rwanda, wakiyawakilisha mataifa yao katika  michezo ya kusaka nafasi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika(Afcon2021) ni wazi kutaongeza mirali ya Wekundu hao wwatakapoikabili Ruvu Shooting.

Upande wake,  Azam itavaana na Mbao FC ikiwa na ari, baada ya kutoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Biashara United, nyumbani kwake  Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mbao itaikaribisha Azam ikiwa na fikra za kutaka kuendeleza ushindi, baada ya  kuitungua  JTK Tanzania bao 1-0, katika mchezo wake uliopita uliochezwa dimba la Meja Jenerali Michael Isamuhyo, Dar es Salaam.

Azam wao wanashika nafasi ya 11 wakijikusanyia pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara saba na kushinda michezo minne huku wakipoteza miwili na kutoa sare moja, wakati Mbao FC wanashika nafasi ya 10 wakijikusanyia pointi 14 wakiwa sawa na Allience wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumzia mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, alisema wanakutana na Ruvu Shooting ambao wameonyesha ushindani kwa timu kubwa hivyo lazima wazidishe umakini.

“Tunahitaji kuendeleza ushindani katika mchezo huu, kwa maandalizi haya tuliyofanya naamini tutashinda,” alisema.

Upande wao, Ruvu Shooting ambayo inayonolewa na Kocha Mkuu,  Salum Mayanga, ilizitaka kwa udi na uvumba pointi tatu ili kuzidi kujongea juu ya msimamo.

“Tumejiandaa kuisambaratisha Simba hivyo wajipange vizuri, mipango yetu ni kuendeleza ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles