31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Simba kuivaa Azam, Yanga vs Kagera Sugar Kombe la FA

 JESSCA NANGAWE– DAR ES SALAAM

MABINGWA wa michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), maarufu kwa Kombe la FA, timu ya Azam wanatarajiwa kukutana na Simba katika mchezo wa robo fainali.

Katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam, Yanga watavaana Kagera Sugar, wakati Sahare All Stars wakimenyana na Ndanda huku timu ya Namungo itapepetana na Alliance.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa timu ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka za Kazi’, alisema mara baada ya droo hiyo kikosi chao kitaendelea kujifua vyema kwa kuwa kina kazi kubwa ya kufanya ikiwamo kutetea taji hilo kwa mara nyingine ili waweze kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kwa sasa timu upo kwenye maandalizi, kwanza tunajiandaa na Ligi Kuu Bara ambayo itarejea Juni 13, mwaka huu, baada ya kusimama mzunguko wa 29 kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona,”

“Malengo yetu ni kuona tunatetea ubingwa wetu wa Kombe la Azam kwa mara nyingine ili tuendelee kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa,” alisema Zaka za Kazi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,612FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles