25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Simba, Kagera kazi haitakuwa rahisi leo

Asha Kigundula -Dar es salaam

MABINGWA watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Simba leo itashuka dimbani kuumana na Kagera Sugar, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba itashuka dimbani ikihitaji kuweka heshima dhidi ya Kagera Sugar ambayo ni moja kati ya timu imara na zenye uzoefu katika ligi hiyo.

Wekundu hao wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wake uliopita ilipoichapa Mwadui FC mabao 5-0, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbloeck huenda  leo akawatumia wachezaji wengi  ambao  hakuwatumia katika michezo iliyopita, lengo likiwa kuwaepusha majeraha, nyota wake tegemeo anapojiandaa kuikabili Yanga Jumamosi.

Simba inashuka uwanjani ikiwa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu,ikiwa imecheza mechi nane, ikitoka sare na kuchapwa michezo miwili, hivyo kukusanya pointi 16.

Kagera Sugar kwa  upande mwingine itaingia dimbani  ikiwa na kumbukumbu safi ya  kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita, Simba iliibuka mbabe dhidi ya Kagera kwenye michezo yote miwili, ikianza kushinda mabao 3-0, mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Septemba 26 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba Bukoba mkoani Kagera kabla ya kushinda bao 1-0, mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Februali 18 mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mbali ya mchezo huo, pia itapigwa michezo mingine miwili, JKT Tanzania itakuwa ugenini Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi kuumana na Namungo, Mwadui itakuwa nyumbani Uwanja wa Mwadui Complex kupepetana na Ruvu Shooting.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles