27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA INAWAPIGA TU

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

SIMBA imekoleza kasi katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, mchezo uliochezwa Uwanja  wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao yote mawili ya Simba  katika mchezo huo yalipachikwa wavuni na beki raia wa Brazil, Gerson Fraga Vieira.

Fraga alifunga mabao yake dakika ya saba na 78.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

Dakika ya pili, mshambuliaji Meddie Kagere alitikisa nyavu za Coastal kwa kufunga bao, lakini mwamuzi alilikataa kwa madai kwamba alikuwa ameotea.

Dakika ya saba, mpira wa adhabu uliopigwa na Chama ulitua kwenye kichwa cha Fraga ambaye aliifungia Simba bao la kuongoza.

Baada ya bao hilo, kosa kosa ziliendelea kila upande.

Kagere na Ibrahim Ajib mara kadhaa walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuiandikia Simba bao, lakini  mashuti yao ama yalitoka nje au kudakwa na kipa wa Coastal Union, Soud Abdalah.

Hali kama hiyo ilionekana kwa upande wa Coastal, kwani washambuliaji wao Ayub Semtawa, Ayub Lyanga na Issa Abushee walishindwa kutikisa nyavu kutokana na kukosa utulivu au mashuti yao kudakwa na kipa wa Simba, Beno Kakolanya.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza, zilikamilika kwa Simba kwenda mapumzikoni ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza, mashambulizi yalikuwa yakupokezana.

Kipindi cha kwanza, kila upande uliingia na uwanjani na nguvu zaidi ikiamini itakuwa njia sahihi ya kupata bao au mabao.

Hata hivyo, Simba ndiyo ilinufaika na mpango mkakati huo baada ya Fraga kufunga bao la pili dakika ya 78, baada kuukwamisha mpira uliotemwa na Abdalah, aliyepangua kiki ya Hassan Dikunga.

Baada ya kufungwa bao hilo, Coastal iliendelea kupambana ili kusaka bao, lakini ukuta wa Simba ulikuwa imara kuondosha hatari zote langoni mwao.

Dakika 90 za pambano hilo, zilikamilika kwa Simba kutakata na ushindi wa mabao 2-0.

Kwa ushindi huo, imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, ikifikisha pointi 47, baada ya kushuka dimbani mara 18, hivyo kusaliwa na mchezo mmoja ili kukamilisha michezo yake ya mzunguko wa kwanza.

Katika mchezo huo, beki wa Simba, Erasto Nyoni  alilazimika kufanyiwa mabadiliko kipindi cha kwanza, baada ya kuumia.

Michezo mingine ya  ligi hiyo, Biashara United ya Mara ikiwa nyumbani Uwanja wa Karume mjini Musoma iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui, Kagera  Sugar ikiwa nyumbani Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ikaitandika Singida United mabao 3-0.

Namungo baada ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Simba kwa kuchapwa mabao mabao 2-1, ikiwa nyumbani Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi ikaisurubu Mbao mabao 3-0, wakati Ruvu Shooting ikiwa nyumbani Uwanja wa Mabatini ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles