27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA INA HATARI

Theresia Gasper, Dar es salaam

TIMU ya Simba imerejea kwenye makali yake, baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya City, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yalipachikwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti dakika ya saba, Clatous Chama dakika ya 43, Sharaf Eldin Shiboub dakika ya 77 na Deo Kanda aliyepigilia msumari wa mwisho dakika ya 86.

Ushindi huo umeirudia Simba  njia  kuu, baada ya kuonja machungu ya kupoteza mchezo,  ilipochapwa  bao 1-0 na Mwadui FC, timu hizo zilipoumana Uwanja Kambarage, Shinyanga.

Simba imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi  hiyo, baada ya kufikisha pointi  21,  ilizovuna kupitia michezo yake nane iliyoshuka dimbani, ikishinda saba na kupoteza mmoja.

Simba iliuanza mchezo kwa kujiamini ikitumia viungo wake watano waliifanya imiliki mpira na kujenga mashambulizi.

Dakika ya sita,  Miraji Athumani aliangushwa ndani ya eneo la hatari la Mbeya City na mwamuzi wa mchezo huo, Athumani Lazi kuamuru ipigwe penalti.

Kagere aliindikia Simba bao la kwanza dakika ya saba  kwa mkwaju wa penalti.

Dakika ya 26, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi alifanya mabadiliko, alimtoa Seleman Mangoma na kumwingiza Majaliwa Shabani.

Dakika 34, Shaban alishindwa kutumia vema makosa ya beki wa Simba, Pascal Wawa  baada ya mpira kumfikia lakini akaachia shuti lililopaa.

Dakika ya 36, Miraj alipoteza nafasi ya wazi kuifungia Simba bao la pili, baada ya kupokea krosi safi ya Kagere, lakini mpira wa kichwa aliopiga uliishia mikononi mwa kipa wa Mbeya City, Richard Peter.

Dakika 43, Chama aliindikia Simba bao la pili kwa shuti kali,  baada ya kuwalamba chenga mabeki watatu ya Mbeya City kabla ya kumtungua Richard.

Kipindi cha kwanza kilimazika kwa Simba kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0, kipindi cha pili kilianza kwa kocha wa Simba, Patrick Aussems kumtoa Miraj na kumwingiza Francis Kahata.

Dakika ya 55, Kagere alipenyezewa pasi maridadi na Kahata na kuachia shuti lililodakwa na Richard.

Dakika ya 60, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Gerson Fraga Viera.

Dakika ya 68, Samson Madeleke wa Mbeya City alilimwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Ibrahim Ajib.

Dakika ya 69, Mbeya City ilifanya mabadiliko, alitoka Richard  na kuingia Mohamed Kapeta.

Dakika 77, Shiboub aliindikia Simba bao la tatu kwa kichwa akimalizia krosi ya Ajib.

Dakika moja baadaye Ajib alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na  Deo Kanda.

Dakika ya 86, Kanda aliifungia Simba bao la nne baada ya kuwazidi kasi mabeki wa Mbeya City na kuachia mkwaju uliokwenda moja kwa moja wavuni.

Dakika 90 za mtanange huo zilikamilika kwa Simba  kuondoka uwanjani  na pointi zote tatu .

Coastal Union ilijikuta ikipokea kichapo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Mbao, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

JKT Tanzania ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Maafande wa Tanzania Prinsons, mchezo uliochezwa Uwanja Meja Jenerali Michael Isamhuyo, Dar es Salaam.

Ndanda ilizinduka nyumbani na kuichakaza Ruvu Shooting mabao 2-0, mchezo uliochezwa Uwanja wa Nagwanda Sijaona, Mtwar, huku Polisi Tanzania ikivuna ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vijana wa Alliance kutoka Mwanza, mechi iliyopigwa Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mbali na mchezo huo, kivumbi kingine cha ligi hiyo kilitimka katika  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles