25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Simba hakuna kulegeza kamba

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems, kimeendelea kujifua kwa mazoezi sambamba na mbinu tofauti kwa ajili ya kuhakikisha kinaitupa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya UD Songo ya Msumbuji.

Wekundu hao watakuwa wenyeji wa UD Songo, katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya ligi hiyo utakaochezwa Jumapili hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza ulichezwa jijini Beira nchini Msumbuji, ambapo Simba ililazimisha suluhu.

Matokeo hayo yanaufanya mchezo wa marudiano kuwa mgumu zaidi kwakua kila upande una fursa ya kusonga mbele, ikiwa utapata ushindi.

Jana asubuhi kikosi cha Simba kiliendelea na mazoezi kwenye Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam, ambapo MTANZANIA lilishuhudia Aussems akitumia muda mwingi kwenye zoezi la kupiga mashuti nje ya 18.

Pia alionekana akiwapika viungo wake Sharaf Eldin Shiboub, Jonas Mkude, Fransic Kahata, Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin, ili kama safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere itabanwa wao watumie mwanya huo kufunga.

Akizungumza baada ya mazoezi yao, Aussems alisema wataingia uwanjani na pango tofauti na ule wa Beira, kwani safari hii watashambulia zaidi ili kusaka mabao na hatimaye waweze kuibuka na ushindi.

“Ugenini tulilenga zaidi kuhakikisha haturuhusu bao na tulifanikiwa, tutakuwa na mpango tofauti kwenye mchezo wa marudiano ambao ni  kushambulia zaidi  kwakua tunahitaji ushindi na si kingine,” alisema raia huyo wa Ubelgiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles