27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

SIMBA BADO WANAOTA NDOTO ZA UBINGWA

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAM


simbaINAWEZEKANA ni mapema mno kuanza kuzungumzia ubingwa, lakini siku zote Waswahili husema ‘biashara asubuhi jioni mahesabu’, wakiamini kuwa msingi bora hujenga nyuma imara.

Kwa kuiangalia kasi waliyoanza nayo Simba katika msimu huu wa 2016/17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ni dhahiri kuwa wamepania kumaliza utawala wa Yanga na Azam.

Baada ya kucheza mechi 19, Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi, ikiwa imeshinda mechi 14 na kutoa sare tatu na kufungwa mbili na kujikusanyia jumla ya pointi 45, pointi mbili juu ya Yanga, inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43, baada ya kucheza michezo 19, wakiwa wamepoteza miwili, sare nne na wameshinda michezo 13.

Kuanza vibaya kwa Yanga na Azam kwenye msimu huu wa ligi, kulitoa nafasi kwa Simba kuanza kuota ndoto zao za kurudisha taji la ligi Msimbazi, lakini kwa sasa mambo yamebadilika.

Awali Yanga baada ya kucheza mechi saba ilishika nafasi ya nne ikiwa na pointi 14, zilizotokana na kushinda mechi nne tu, kutoka sare mbili, huku ikifungwa mchezo mmoja.

Wakati huo Yanga ilikuwa na tofauti ya pointi nane dhidi ya vinara Simba, ambao walionekana kuwa imara zaidi.
Lakini kwa sasa timu hizo zinatofautiana kwa pointi mbili tu na tayari Simba wameanza kurudi nyuma wakifikiria kwamba huenda msimu huu pia ukapita bila mafanikio.

Kuanza kusuasua kwa timu hiyo kunaifanya Yanga walioanza vibaya, kuwa na jeuri ya kutembea kifua mbele wakijigamba kuutetea ubingwa msimu huu.

Simba wana miaka minne tangu wafanikiwe kunyakuwa taji hilo ambalo linaonekana kuwasumbua akili baada ya mahasimu wao Yanga kuwa na mafanikio zaidi.

Zaidi ni kwamba bado mashabiki wa timu hiyo wanaendelea kuonesha sapoti mwanzo mwisho kwa timu yao.
Kwani tangu kuanza kwa msimu huu, wanachama na mashabiki wa Simba wamekuwa wakiisapoti timu yao kwa kiasi kikubwa, ikiwa ni pamoja na kuchangishana na kutoa bonasi kwa wachezaji katika mechi ambazo wanaibuka kidedea, kitu ambacho kimeongeza hamasa ndani ya timu.

Hivyo basi, kama Simba inataka kuendelea kutikisa msimu huu, wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kuendelea kuisapoti timu yao katika hali zote, hata wakati itakapoteleza sababu kwa kufanya hivyo, kutaendelea kuwapa wachezaji nguvu ya kupambana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles