25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Simba, Azam zatunishiana misuli

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM 

BAADA ya kupanga kukutana katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), timu ya Simba na Azam, kila mmoja ameonekana kuweka mikakati ya kusonga mbele.

Michezo ya robo fainali inatarajia kuchezwa mwishoni mwa mwezi ujao na timu zote zimeanza mazoezi.

Timu nyingine zilizotinga hatua hiyo ni Yanga itakayokutana na Kagera Sugar, Ndanda dhidi ya Sahare All Stars, Namungo FC itacheza na Alliance FC.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema itakuwa ni mechi ngumu na mzuri kutokana na uimara wa timu zote mbili.

Sven alizungumza hayo kupitia tovuti ya Simba na kukiri kuwa ni mechi ya kisasi kutokana na kuwafunga Azam katika michezo yote msimu huu.

“Ninavyoona itakuwa ni mechi ya kisasi na ngumu, ukiangalia Azam ni timu nzuri kama ilivyo Simba japo tuliwafunga katika mechi mbili za ligi, lazima watataka kulipiza kisasi,” alisema Sven.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Bahati Vivier, alisema watafanya maandalizi mazuri ili kujipanga kuendelea katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

“Ratiba tumeiona, tumejipanga kufanya mazuri ili tuwatoe Simba na tuone kama tunaweza kuendelea na safari yetu, nina imani tukijiweka vizuri benchi la ufundi, tukaandaa timu ikawa tayari kutafuta ushindi, mechi itakuwa nzuri.

“Kwenye Ligi tumekutana mara mbili wakafanikiwa kutufunga, lakini nasema hii sio ligi ni mechi moja inayotaka timu moja itoke, tutafanya mipango tuwatoe ili kulipa kisasi,”alisema Bahati.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles