25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Silinde aweka rehani vyeo wakuu wa shule, Maafisa elimu Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, David Silinde, amewataka Maafisa Elimu Sekondari na Wakuu wa shule ambazo hazijakamilisha ujenzi wa mabweni mkoani Simiyu kuhakikisha ifikapo Aprili 31,2021 wawe wamekalimisha ujenzi huo na wakishindwa watapoteza nafasi hizo.

Silinde ametoa maagizo hayo leo Machi 6, baada ya kutembelea baadhi ya shule katika Wilaya za Itilima na Bariadi kujionea ujenzi huo, ambapo shule zote alizotembelea ameshangaa kukuta ujenzi ukiwa bado haujakamilika huku fedha zikiwa zimeisha.

Naibu Waziri huyo amesema serikali ilitoa kiasi cha Milioni 80 katika baadhi shule kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ili kuwasaidia wanafunzi walioka katika mazingira magumu na hatarishi hasa wanasichana.

Amesema kuwa katika mikoa mingine ujenzi umekamilika wa mabweni kwa kiasi hicho cha fedha, lakini katika mkoa wa Simiyu ameshangazwa kuona ujenzi ukiwa bado haujakamilika lakini na fedha zote zimeisha.

Naibu Waziri huyo ametembelea shule za Sekondari Itilima iliyoko Wilayani Itilima, Nyasosi na Bariadi zilizoko Wilayani Bariadi, amewataka wakuu wa shule hizo maafisa elimu wa halmashauri kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa muda aliotoa au watavuliwa nyazifa zao ikiwa watashindwa.

“Haiwezekani katika Mikoa mingine wakamilishe kwa fedha hizo hizo, lakini Simiyu mmeshindwa, kwanza kama serikali hatutaleta fedha nyingine…pili tunataka ujenzi ukamilike na halmashauri ziwajibike kutafuta fedha za kukamilisha,” amesema Silinde…

“Hadi kufikia Aprili 31, 2021 ujenzi ukamilike na wanafunzi waanze kutumia, mkishindwa mkuu wa shule na afisa elimu hamtakuwa na nafasi hizi tena, hatuwezi kuvumilia hali hii, kuna dalili kuwa fedha za serikali zimetumika vibaya,” amesema Silinde.

Mbali na hilo amewataka wakuu wa shule hizo, maafisa elimu ndani ya siku tatu kutoa maelezo ya maandishi ya kwa nini wameshindwa kukamilisha ujenzi huo ikiwa pamoja na kuonyesha ghamara walizotumia.

Aidha amesema kuwa tatizo kubwa lipo kwa waandisi wa halmashauri, ambao wamekuwa wakitoa michoro yenye gharama kubwa.

Kwa upande wao wakuu wa wilaya hizo Festo Kiswaga Bariadi na Benson Kilangi, walihaidi kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa maagizo ya Waziri hasa kuhakikisha ifikapo Aprili 31, ujenzi unakamilika.

“Kama Mkuu wa Wilaya nitahakikisha ujenzi huu unakamilika ndani ya muda ambao umetoa, lakini tutaendelea kusimamia ujenzi huu kuhakikisha unakuwa kwenye ubora na hakuna fedha yeyote itakayoliwa,” amesema Kiswaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles