27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

SILAHA HARAMU 5,608 ZATEKETEZWA KIGOMA

Na EDITHA KARLO, KIGOMA


silahaWAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameongoza uteketezaji wa silaha haramu 5,608 zilizosalimishwa au kukamatwa kwenye matukio ya uhalifu na   ambazo hazifai kutumika.

Hatua hiyo ilitekelezwa jana Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Ujiji kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani.

Waziri Mwigulu aliwataka wananchi kushirikiana na Serikali kuwafichua watu wanaomiliki silaha kinyume cha taratibu na sheria kwa sababu   ni wazi hawana nia njema na amani ya nchi.

Alisema tatizo la kuzagaa silaha ni tatizo la dunia nzima, hivyo ni vema wananchi wakashirikiana na vyombo vya dola kuzizuia kuzagaa holela nchini.

“Ndugu zangu madhara ya kuzagaa silaha holela yapo mengi ikiwa ni pamoja na kuathiri maendeleo ya nchi katika uchumi, siasa na jamii.

“Pia kunachangia vitendo vya uhalifu, hivyo kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake,” alisema.

Mwigulu alisema Tanzania inaungana na umma wa Umoja wa Mataifa kupiga vita kuzagaa silaha ndogo na nyepesi nchini.

Alisema hivi karibuni ulifanyika uhakiki wa silaha na asilimia 62.16 ya wamiliki halali walihakikiwa, huku asilimia 37.84 hawakuhakikiwa.

Mwigulu alisema itakapofika Juni 30, mwaka huu, leseni zao zitakoma kwa mujibu wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi.

“Muda huo ukiisha wale wote ambao hawajafanya uhakiki wa silaha zao watasakwa popote walipo na watakamatwa na kufikishwa kwenye sheria kwakuwa watakuwa wanamiliki silaha kinyume cha sheria,” alisema.

Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani Mssanzya alizitaja   silaha haramu zilizoteketezwa ambazo hazifai kutumika kuwa ni bastola 21 na shotgun 606.

Nyingine ni SMG 166, rifle 300, FN rifle tatu, magobore 4,487, G3 moja na SRA tatu.

Alisema uteketezaji ulifanyika Mkoa wa Kigoma kwa sababu takwimu za uhalifu zinaonyesha mikoa ya ukanda huo ndiko   silaha nyingi za haramu hukamatwa katika matukio mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles